loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Shule yakabidhiwa mradi wa mil. 600/-

Hafla ya makabidhiano ya mradi huo ilihudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia aliyemwakilisha mke wa Rais, Mama Salma Kikwete.

Kadhalika, hafla hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Wilman Kapenjama, maofisa kutoka Ofisi ya Elimu Mkoa pamoja na wananchi mbalimbali.

Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi huo, Waziri Ghasia aliwashukuru na kuwapongeza Ophir Energy kwa mabadiliko makubwa chanya waliyoifanyia shule hiyo kwa kuwapatia wanafunzi na walimu mazingira bora ya kujifunza na kufundishia.

Ghasia alivutiwa pia na ukweli kwamba kazi za mradi huo zilifanywa na makandarasi wazalendo, ambapo alisema:

"Hii ni ishara nzuri sana kwa sababu inaonesha wazi malengo ya Ophir na Sera ya Tanzania kuhakikisha kwamba wawekezaji wanawezesha biashara za ndani katika maeneo walipo."

Aliwaomba wanajumuiya wa shule hiyo kutunza vyema majengo na kuahidi kufanya ufuatiliaji wa karibu juu ya utendaji wa wanafunzi shuleni hapo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwakilishi wa Bodi ya Ophir, Mkurugenzi asiye Mtendaji, Vivien Gibney alisema;

"msaada kwa Lilungu unalenga kupandisha kiwango cha elimu katika Mkoa wa Mtwara pamoja na kuunga mkono jitihada za serikali katika kutoa elimu bora Tanzania."

Alisema programu hiyo ilijumuisha ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa, jengo moja la ofisi katika jengo C na D, uchimbaji wa kisima kipya chenye mashimo 16 na ujenzi wa mnara wa maji.

Alisema msaada wa ziada kwa shule hiyo ulijumuisha utoaji wa madawati 240 kwa ajili ya madarasa husika, uwekaji wa matangi ya maji yanayohifadhi lita 50,000 na kusawazisha sawa viwanja vya shule.

RAIS John Magufuli amewataka wasaidizi wake ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi