loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Shule za msingi Kilwa taabani

Ofisa Elimu wa Shule za Msingi wilayani Kilwa, Lezira Maira alithibitisha hayo wakati alipokuwa akizungumza na HabariLeo ofisini alisema kuwa shule kwa jumla za msingi ziko katika wakati mgumu, zinatofautiana kimatatizo kuna shule ina upungufu wa vyoo, nyingine madarasa, au zimeondolewa mabati na ukosefu wa nyumba.

Alisema kwa hiyo mamlaka husika inafanya juhudi mbalimbali kuweza kukabiliana na matatizo hayo.

Hata hivyo alisema kuwa Serikali Kuu iliweza kutoa Sh milioni 200 mwaka huu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu, lakini kuna kiasi cha fedha zilichukuliwa kuweza kukarabati shule.

Maira alisema kuwa hivi sasa kuna ukarabati wa Shule ya Msingi ya Songa Mnara ambayo ilikuwa haina vyoo sasa vinajengwa ambayo iko katika maeneo ya baharini, wilayani humo.

Aliongeza tatizo lililokuwapo kwa jamii kuwa shule ni mali ya Serikali siyo za umma, kwani hata wale waliosoma kwenye mashule hayo na maofisa hawataki hata kuchangia juu ya elimu katika shule hizo.

Naye Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi ya Miteja, Mwajabu Kipatimu, alisema kuwa shule hiyo ilianzishwa mnamo mwaka 1948.

Alisema kuwa kuna upungufu wa matundu 16 ya vyoo. Alisema kuwa wapo wanafunzi wapatao 441 kwa hiyo mahitaji yao kuwa na matundu 20.

MABALOZI wawili wa nchi za Marekani na Vietnam waliowasilisha hati ...

foto
Mwandishi: Kennedy Kisula, Kilwa

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi