loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Si kila aliyefanikiwa kimaisha anastahili kuigwa

Vijana wengi hutafuta mtu aliyefanikiwa ili aweze kuwa motisha na kuwatia moyo kufanikiwa, hili ni jambo zuri maana wako wengine wamefanikiwa sana kutokana na kuona kuiga watu waliodhani kuwa ni muongozo wao katika kufanikisha mambo katika maisha yao.

Hata hivyo, tatizo linakuja vijana wengi wanatafuta watu wa kuwaangalia kama mfano lakini kwa kuangalia hali ya sasa ya mhusika badala ya kuangalia yule mhusika hadi alivyofanikiwa safari yake ilianzia wapi hadi kufika hapo alipo.

Unapomuangalia mtu ambaye unamuona kama mfano wa kuiga kwa kuangalia hali ya sasa halafu ukasahau kuangalia safari yake unaweza kujikuta umeiga mtu ambaye kwa uhakika hafai kukuhamasisha kabisa.

Kutokana na mtazamo au dhana iliyojengeka kulingana na hali ya maisha ya sasa watu wanafurahia watu wenye fedha, vyeo na madaraka bila kujali vimepatikana vipi, kwa njia gani na kwa juhudi zipo.

Watu wanaangalia mwisho wa safari, lakini safari ilianzia wapi, changamoto alizokutana nazo hadi kufikia hapo hapana! Haya mambo ya kutaka harakaharaka ya mafanikio imepelekea vijana wengi kuangalia watu ambao kimsingi sio hasa wanaoweza kuwasaidia kufikia malengo yao.

Vijana ambao wanaanza kuingia katika maisha sasa wamekuwa wakijikuta wanatazama mifano ya watu waliofanikiwa katika jambo fulani bila kujiuliza maswali mengi au kutaka kufahamu kwa undani huyo wanayemtazama ameanzia wapi safari ya mafanikio.

Unakuta mtu anamuangalia huyo anayemchukulia kama ‘role model’ ambaye kwa uhakika ukiangalia maisha yake hakuna hata kimoja kinachopaswa kuigwa, kwa sababu mtu huyo mafanikio yake yametokana na njia nyingi sana za mkato ambazo hazipendezi.

Lazima vijana kujijengea tabia ya kufanya utafiti ama uchunguzi wa jambo lolote kabla ya kuchukua hatua ya kulifanya ama kuiga kwa mtu bila kufahamu kwa undani ameweza kufanikiwa kwa njia gani.

Hii tabia ya kushabikia watu kwa sababu unaona ana fedha, anaendesha magari ya kifahari, ana safiri sana, kajenga nyumba za kifahari au anatoa sana misaada bila kufahamu amefikaje hapo, unaweza kujikuta unadondokea sehemu ambayo baadye ikaja kukugharimu maisha yako baadaye.

Haina maana hatupaswi kutazama watu waliofanikiwa kama mfano la hasha, jambo la msingi nikufahamu vyema amefanikiwa kwa njia gani, ametokea wapi hadi kufikia hapo alipo, ukifahamu safari yake vizuri ya mafanikio itakusaidia kukujenga hata wewe hatua kwa hatua hadi nawe ukafikia malengo katika maisha.

Unachotakiwa ni kujifunza kutoka kwa wale waliotutangulia kwa kuangalia mwenendo wao na kujifunza jinsi wanavyofanya kazi kwa bidii, wanavyotumia fursa vizuri na wanavyojua kuokoa muda lakini yote yawe katika kumpendeza Mungu hilo usisahau.

Kwa nini nasema yawe katika kumpendeza Mungu, maana siamini kama aliyefanikiwa mfano kwa kufanya ujambazi, wizi, rushwa, dhuluma, udanganyifu na mambo kama hayo anaweza akawa mtu wa kuigwa na kusema amefanikiwa hata kama amekwisha acha lakini aliyafanya maovu hayo ndio akapata hayo mafanikio unayotaka kuyafikia na wewe.

Kuna watu wanafaa kuigwa sana na wewe kijana, lakini kwa sababu hawatangazwi, hawajionyeshi, hawajulikani basi vijana wanaona kama hawafai.

Hebu leo jaribu kutazama watu wa kawaida tu wanaokuzunguka, unaweza kushangaa wako wengi sana unaoweza kuwatazama kama mfano wa kuigwa na ukajifunza jambo kwao na ukaweza kutoka hatua moja uliopo sasa na kufika hatua nyingine kwa kutazama hata mafanikio yao madogo.

UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Riadha ...

foto
Mwandishi: Angela Semaya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi