loader
Dstv Habarileo  Mobile
Sijawasaliti wakazi wa Tarime - Mbunge

Sijawasaliti wakazi wa Tarime - Mbunge

Mbunge huyo amesema pia hajajenga hoteli yoyote ndani ya SENAPA na kwamba uvumi huo hauna ukweli na unalenga kumchafua kisiasa. “Mimi sijahongwa na siwezi kuhongwa. Wala sina hoteli ndani ya hifadhi.

Huu ni uongo mtupu”, alisema hayo Nyambari katika mkutano na waandishi wa habari juzi. Alisema yuko pamoja na wananchi wake waliopitiwa na Operesheni Tokomeza Ujangili ambayo imewang’oa kazini mawaziri wanne.

Mbunge huyo aliwataka wananchi hao kuwa wavumilivu na kuendelea kuheshimu sheria wakati juhudi za kutatua mgogoro uliopo kati yao na SENAPA zinaendelea.

“Niko pamoja na wananchi wangu wote, Operesheni Tokomeza ilifanyika nchi nzima. Niombe wafuate sheria”, Nyambari ambaye pia ni mjumbe wa Bodi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).

Mamia ya wakazi wanaoishi jirani na SENAPA wamekuwa katika mgogoro wa muda mrefu na TANAPA, wakilalamikia shirika hilo lenye dhamana ya kulinda na kuhifadhi hifadhi za taifa kuweka mipaka ambayo wanadai imemega eneo la bonde la Nyanungu .

Wananchi hao kwa sasa wanadai hawana sehemu ya kulishia mifugo yao baada ya mipaka hiyo kuwekwa jambo ambalo limesababisha mvutano mkali kati yao na wahifadhi katika miezi ya hivi karibuni.

Siku chache zilizopita maofisa wa SENAPA walikamata zaidi ya mifugo 500 iliyokuwa kwenye malisho ndani ya bonde la Nyanungu, eneo ambalo Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, William Mwakilema anasisitiza kuwa ni sehemu ya hifadhi.

Mwakilema pia amekaririwa kwenye vyombo vya habari mara kwa mara akiwaomba wananchi hao kuheshimu mipaka iliyopo kwa sasa, jambo ambalo wananchi hao wanaona linawaweka katika hali ngumu ya maisha.

RAIS wa Zanzibar,  Dk Hussein Mwinyi amesema wakati umefika kwa ...

foto
Mwandishi: Mugini Jacob, Tarime

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi