loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba kuamua hatima ya Wambura

Mkutano huo unatarajia kufanya marekebisho ya baadhi ya vipengele kwenye Katiba yao pamoja na kujadili wanachama 71 waliokwenda mahakamani kinyume cha sheria za soka.

Kufanyia marekebisho ya Katiba ni moja ya ahadi ya Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva wakati alipochaguliwa baada ya kubaini kuwepo kwa mapungufu, akilenga kuleta umoja.

Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, Makamu wa Rais wa klabu hiyo, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ alisema Katiba iliyopo inamnyima fursa Rais kufanya uteuzi wa wajumbe, akidai iliyopo inasema wajumbe wa kuteuliwa lazima wawe na sifa ya wale waliochaguliwa.

“Kama mnakumbuka Rais wetu alipochaguliwa aliahidi kufanya marekebisho ya Katiba sasa tunaelekea kufanikisha hayo,” alisema Kaburu.

Aidha, wanachama 69 waliokwenda mahakamani kwenye mchakato wa kupinga uchaguzi kabla haujafanyika Uchaguzi Mkuu Juni 29, mwaka huu, na wengine wawili wa mwaka 2010 akiwamo Michael Wambura, wote watajadiliwa kwenye mkutano huo.

Hivi karibuni, Rais mstaafu wa Simba, Ismail Aden Rage alimshauri Rais mpya, Aveva kuwasamehe wote waliokwenda mahakamani kama kweli anataka kuleta umoja kwa wanachama wa Simba.

Jambo hilo, Aveva alisema amelipokea, lakini atalipeleka kwa Kamati ya Utendaji kuona kwamba itakuwaje na sasa imetangazwa kujadiliwa kwenye mkutano wao huo kupata suluhu. Kaburu alisema wanachama wote waliopewa barua watahitajika kufika kujibu yale watakayoulizwa.

TIMU ya Ruvu Shooting imeboresha kikosi ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi