loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Simba yabuni mpango wa kuongeza mapato

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Rage alisema katika kutimiza mpango huo, tayari ameanza mazungumzo na Benki ya Posta Tanzania (TPB) kwa ajili ya kutengeneza kadi maalumu kwa mashabiki wa Simba, lengo likiwa ni kuchangia kupitia benki hiyo.

“Tumeanzisha kadi hizo ambapo tunataka tuwe na data kwa mashabiki wote wa Tanzania wa klabu yetu, kujenga utamaduni wa kuchangia, lakini itatusaidia kujua tuna mashabiki wangapi,” alisema Rage.

Alisema anategemea kukutana na uongozi wa benki hiyo kwa mara ya mwisho kabla ya kumalizika kwa wiki hii, ili wiki ijayo wasaini mkataba, kwa ajili ya kufanikisha mpango huo.

Rage alisema mpango huo ukifanikiwa, utatoa fursa kwa kila shabiki kujitokeza katika benki hiyo na kujaza fomu kisha kuchangia Sh 10,000 zitakazoingia katika akaunti ya klabu na kusaidia kuboresha mapato yao.

Alisema sababu kubwa ya kuanzisha mpango huo ni baada ya kugundua kuwa gharama za kuendesha klabu zimekuwa ni kubwa kuliko uwezo wao na kuongeza kuwa kutegemea fedha za wafadhili na mapato ya uwanjani hazitoshi peke yake bila kutafuta vyanzo vingine vya mapato.

Alisema kwa mwezi wamekuwa wakitumia Sh milioni 52 kwa ajili ya kulipa mishahara, wakati fedha za wadhamini hupewa Sh milioni 30, kiwango ambacho anasema hakitoshi kutimiza haja zao.

“Kwa mfano tulikutana na Mgambo juzi, mapato tuliyopata ni Sh milioni nne, na sisi tulisafiri kwa Sh milioni 15, ukijumlisha na hoteli ilifikia milioni 20, ilibidi tukope fedha za kurudi Dar es Salaam,” alisema.

Akizungumzia sababu za mashabiki kupungua uwanjani, alisema anafikiri kiwango cha wachezaji kufanya vibaya ni mojawapo, lakini pia tiketi za elektroniki na zaidi hali ya maisha za mashabiki kwa kipindi hiki ni kigumu ndio maana wengi hawafiki uwanjani.

Pia, alisema mpira wa nje unachangia wengi kutothamini Ligi Kuu, kwani wengi hupenda kufuatilia zaidi huko, wakiacha huu wa nyumbani.

KOCHA wa Yanga, Cedric Kaze amewashusha ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi