loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Sitta aweka mambo sawa

Alifafanua kwamba hatua hiyo ni mawasiliano ya kawaida, yanayohusu safari kutoka Rasimu Mpya ya Katiba mpaka kufikia katika Katiba Mpya inayopendekezwa ipatikane.

“Jambo lolote lililoandikwa na binadamu halikosi kasoro, katika Rasimu hii ya Katiba tumegundua inayo upungufu kadha wa kadha, kuna baadhi ya maoni ambayo hayakuzingatiwa ndiyo maana tunayafanyia kazi ili yawemo katika Katiba Mpya itakayopatikana,” alisema Sitta.

Sitta alisema hayo jana katika mkutano wake na baadhi ya viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (Shivyawata), mjini hapa.

Aliwahakikishia watu wenye Ulemavu nchini, kuwa wanatendewa haki katika Katiba Mpya itakayopatikana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Inclusive Development Promoters and Consultants kutoka Dar es Salaam, Kaganzi Rutachwamagyo alisisitiza kuwepo uwakilishi wa watu wenye ulemavu kwenye Bunge, Baraza la Wawakilishi na Mabaraza ya Madiwani kwa kutamkwa kwenye Katiba.

RAIS John Pombe Magufuli anaongoza kwenye ...

foto
Mwandishi: Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi