loader
Dstv Habarileo  Mobile
SMZ kuendelea kulea watoto yatima

SMZ kuendelea kulea watoto yatima

Aidha amesema anaamini Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuwajali watoto wanaotunzwa katika vituo vya kulelea watoto ikiwamo vijiji vya SOS na kuwapa upendo na huduma zote zinazostahili.

Mama Shein aliyasema hayo wakati aliposhiriki katika futari ya pamoja na watoto wanaolelewa katika kituo hicho kilichopo eneo la Mombasa, nje kidogo ya mji wa Unguja.

Alisema watoto wanaotunzwa katika nyumba hizo wanahitaji upendo wa hali ya juu pamoja na kupata huduma zote muhimu za elimu kwa ajili ya kuandaliwa kuwa viongozi wa baadaye.

Alisema uamuzi wa kutunza watoto waliopoteza wazazi wao ni matokeo ya hatua zilizochukuliwa na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume wakati alipoanzisha nyumba kama hizo eneo la Forodhani mjini hapa.

“Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea utaratibu wa zamani wa kuwatunza watoto na kuhakikisha wanapata haki zote na fursa za malezi na matunzo kwa mujibu wa sheria za nchi na za kimataifa,” alisema.

Mapema Mkurugenzi Mkuu wa kijiji cha SOS, Salum Abdalla alisema wamefarajika kuona kijiji hicho kinatembelewa na viongozi mbalimbali wa ngazi za juu serikalini.

Alisema amefurahishwa na uamuzi wa viongozi hao akiwemo Mama Shein pamoja na mke wa Makamu wa Pili wa Rais, Mama Asha Suleiman Iddi kwa kitendo chao cha kujumuika kwa futari na watoto hao ambacho kinatoa mapenzi makubwa kwa watoto hao.

Alisema kituo hicho tangu kilipoanza kazi mwaka 1993 kinaendelea na majukumu yake ya kutoa elimu pamoja na kutunza watoto ambao wamepoteza malezi ya wazazi kwa sababu mbali mbali.

Mtoto anayetunzwa katika kijiji hicho, Fatuma Ahmed (18) alisema fursa zote muhimu wanazipata katika kijiji hicho ikiwemo elimu.

“Sisi watoto tunaotunzwa katika kijiji hiki hakuna huduma tunazozikosa hapa, tunasoma kwa kadiri ya uwezo wetu ambapo shule ya sekondari ipo katika eneo la kijiji,” alisema Fatuma.

MKUU wa Chuo cha Uhasibu Arusha ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi