loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

SMZ kutoa kipaumbele masomo ya gesi, mafuta

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Ardhi Makaazi Maji na Nishati, Haji Mwadini wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura, Hamza Hassan Juma (CCM) aliyetaka kujuwa mikakati ya Serikali kusomesha vijana katika masomo ya gesi na mafuta.

Mwadini alisema Wizara ya Ardhi na Makaazi Maji na Nishati kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu imepanga kutoa kipaumbele zaidi kwa wanafunzi watakaopenda kusoma masomo ya sayansi ya rasilimali ya gesi na mafuta.

Alisema juhudi hizo zimechukuliwa na Bodi ya Mikopo ya Zanzibar ambayo imetoa kipaumbele kwa wanafunzi kuchukua masomo ya sayansi ya mafuta na gesi.

Alizitaja baadhi ya nchi ambazo zimekubali kutoa mafunzo kwa ajili ya wanafunzi wa masomo ya sayansi ya rasilimali ya mafuta ni pamoja na nchi ya Kiarabu ya Rasilkhema ambayo imeahidi kusomesha zaidi ya vijana 13.

“Tumeanza kazi ya kuwahamasisha wanafunzi wa Kidato cha Sita kuchukuwa masomo ya sayansi ya mafuta na gesi kwa sasa kwa sababu mahitaji yake ni makubwa,” alisema.

Aidha alisema jumla ya wanafunzi 29 wanasoma nje ya nchi katika vyuo mbalimbali masomo ya nishati ya mafuta na gesi.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanza kusomesha vijana wake katika fani ya mafuta na gesi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuchimba rasilimali hiyo ambayo inadaiwa ipo katika baadhi ya maeneo ya Kisiwa cha Unguja na Pemba.

Mapema Waziri wa Ardhi Makaazi Maji na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban alisema baadhi ya nchi washirika wa maendeleo ikiwemo Norway imeonesha nia ya kuisaidia Zanzibar kuhakikisha inafanikisha malengo ya kuimarisha sekta ya mafuta na gesi kwa maslahi ya Wazanzibari.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto ...

foto
Mwandishi: Khatibu Suleiman

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi