loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

SMZ yajivunia kudhibiti magendo ya karafuu

Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko, Nassor Ahmed Mazrui alisema hayo wakati alipozungumza na gazeti hili kuhusu uvunaji wa karafuu unaoendelea Pemba.

Alisema Serikali imejizatiti kudhibiti magendo ya karafuu kwa kuwashirikisha wananchi kupitia ulinzi shirikishi na vikosi vya ulinzi vya serikali.

“Tumefanikiwa kupambana na magendo ya karafuu ambayo yalishamiri katika miaka kumi iliyopita kwa wafanyabiashara hao kusafirisha karafuu nchi jirani ya Kenya,” alisema.

Alisema ulinzi umeimarishwa zaidi katika maeneo yote yenye bandari bubu ambazo zimekuwa zikitumiwa na wafanyabiashara wa magendo kusafirisha karafuu nje ya nchi.

Uchunguzi wa gazeti hili uliofanywa umebaini kwamba maeneo mengi ya kisiwa cha Pemba zaidi yanayozalisha kiwango kikubwa cha karafuu yameimarishwa ulinzi ikiwemo kuwekwa vizuizi katika barabara kwa ajili ya ukaguzi.

Shirika la Taifa la Biashara (ZSTC) tayari imefanikiwa kununua jumla ya tani za karafuu 1,220 katika kipindi cha mwezi mmoja tangu kuzinduliwa kwa msimu wa mavuno ya karafuu Pemba.

MCHICHA ni aina nyingine za ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi