loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

SMZ yavunja mashirika yanayojiendesha kwa hasara

Mashirika hayo ni Shirika la magari pamoja na Shirika la Utalii la Zanzibar.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Fedha, Omar Yussuf Mzee wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya bajeti ya Wizara ya Fedha kwa mwaka wa fedha 2014- 2015 katika Baraza la Wawakilishi.

Alisema kutokana na sekta binafsi kuchukua nafasi kubwa katika maendeleo ya biashara, mashirika hayo yalishindwa kujiendesha kibiashara na Serikali kuchukua uamuzi wa kuyafunga.

Alisema uamuzi uliochukuliwa na Serikali kwa sasa ni wafanyakazi wote waliokuwa wakifanya kazi katika mashirika hayo kupangiwa kazi sehemu nyingine kwa mujibu wa taratibu za Serikali.

Aidha alisema uamuzi huo umepata baraka za rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein. Alifafanua zaidi alisema Shirika la Magari limeshindwa kujiendesha kutokana na ushindani mkubwa wa kibiashara uliopo sasa.

Alisema shirika hilo lilishindwa na kubakia kufanya kazi ya kuagiza vyerahani pamoja na baiskeli kazi ambayo inafanywa na watu binafsi. “Shirika la Serikali haliwezi kufanya kazi ya kuuza baiskeli au vyerahani katika kipindi cha mabadiliko ya biashara huria kwa sasa,”alisema.

Aidha kwa upande wa Shirika la Utalii Zanzibar limeshindwa kufanya kazi kutokana na sekta binafsi kufanya kazi kubwa ya kutembeza na kupokea watalii nchini.

Mzee alisema kazi ya Shirika la Utalii kwa sasa itakuwa ikifanywa na Kamisheni ya Utalii nchini pamoja na sekta binafsi ambayo mchango wake katika kuendeleza sekta hiyo ni mkubwa sana.

RAIS John Magufuli amewataka wasaidizi wake ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi