loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Soko la zabibu bado finyu

Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi, wakati alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mji Mkongwe, Muhammad Ibrahim Sanya(CUF).

Katika swali lake, Sanya alitaka kujua kama Serikali haioni ni wakati muafaka wa kutafuta soko la uhakika la zabibu ili kuondokana na adha wanayoipata wakulima wa zao hilo.

Aidha Mbunge huyo alitaka kujua Serikali itawahamasishaje wakazi wa Mkoa wa Dodoma na maeneo mengine yanayolima zabibu kuongeza uzalishaji ili waweze kufaidika na zao hilo tofauti na ilivyo sasa.

Zambi alisema Serikali kupitia wizara yake imeendelea kuwahamasisha wakulima kuongeza uzalishaji, lakini pia kujiunga na vikundi vya ushirika ili waweze kupata mikopo kwa urahisi na kufanya kilimo hicho kuwa na tija.

Alisema wizara ina mkakati wa kuhamasisha wakulima mkoani Dodoma na maeneo mengine yanayolima zao hilo kwa kutumia kituo cha Utafiti cha Hombolo kwa kuzalisha mbegu.

Katika swali la msingi, mbunge huyo alitaka kujua kwa nini Serikali hailifufui shamba lake la zabibu lililopo Makutupora mjini Dodoma na kuotesha mbegu za zabibu za mezani badala ya zabibu kali tu.

Akijibu swali hilo, Zambi alisema Serikali inaendelea na mikakati ya kufufua shamba la zabibu Makutupora kwa kuweka miundombinu ya umwagiliaji kwa njia ya matone ili kuweza kupata matawi ambayo yatatoa mbegu za zabibu za mezani kwa wingi.

Alisema kituo cha Makutupora mwaka jana kilizalisha na kuisambaza kwa wakulima mkoani Dodoma,Tabora, Wilaya za Bunda na Iringa miche 26,000 kati ya hiyo 3,000 ni ya zabibu za mezani na mwaka huu kinatarajia kuzalisha miche ya zabibu za mezani takribani 50,000.

KAMPUNI ya uchimbaji ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi