loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Stars pumzi muhimu leo

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam wiki mbili zilizopita, timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.

Mchezaji wa Stars, Khamis Mcha ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo huo baada ya kuifungia Stars mabao mawili, wakati huo akiwa ameingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mrisho Ngasa.

Kutokana na matokeo hayo, Stars inahitaji ushindi ugenini leo au sare ya mabao 3-3 ili kupiga hatua mbele.

Ikiwa watafungwa na wenyeji kuanzia sare ya 1-1, watawanufaisha wapinzani wao, lakini wakitoka sare ya 2-2 basi mshindi atapatikana kwa mikwaju ya penalti.

Akizungumza jana baada ya kutua Maputo nchini humo, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij alisema anakiamini kikosi chake ambacho kinacheza mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika dhidi ya Msumbiji (Mambas).

“Nakiamini kikosi changu kitacheza vizuri zaidi kuliko kilivyofanya jijini Dar es Salaam kwa vile hakitakuwa katika shinikizo la mashabiki ambalo mara nyingi hufanya wachezaji wasijiamini,” alisema kocha huyo Mholanzi.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, ilifanya maandalizi yake mwisho nchini Afrika Kusini, na jana katika Uwanja wa Taifa wa Zimpeto ambao ndiyo utakaotumika kwa mechi ya leo.

Stars ilifika hatua hii baada ya kuitoa Zimbabwe kwa jumla ya mabao 3-2, ikishinda 1-0 nyumbani na sare ya 2-2 Harare. Ikiwa itafanikiwa kuwatoa Msumbiji kwenye mchezo huo, itaingia kwenye Kundi F lenye timu za Cape Verde, Niger na Zambia.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) aliye na timu Msumbiji, Boniface Wambura alisema jana kuwa wachezaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu tayari wameungana na wachezaji wengine wakitokea Lubumbashi katika klabu yao ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Alisema mechi itakayochezeshwa na waamuzi kutoka Uganda wakiongozwa na Dennis Batte, itaanza saa 9 alasiri kwa saa za huko ambapo nyumbani Tanzania itakuwa saa 10 jioni.

Wachezaji waliopo katika kikosi cha Taifa Stars Maputo ni Aggrey Morris, Aishi Manula, Amri Kiemba, Deogratias Munishi, Erasto Nyoni, Haruna Chanongo, Himid Mao, John Bocco na Kelvin Yondani.

Wengine ni Mcha, Samata, Mwinyi Kazimoto, Mrisho Ngasa, Nadir Haroub, Oscar Joshua, Ramadhan Singano, Said Moradi, Shabani Nditi, Shomari Kapombe, Simon Msuva na Ulimwengu.

Wakati huo huo, timu ya vijana ya chini ya miaka 17, Serengeti Boys imefungwa mabao 4-0 na Afrika Kusini jana katika mechi ya marudiano ya raundi ya pili iliyochezwa Soweto.

TIMU ya Ruvu Shooting imeboresha kikosi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi