loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

'Suarez asifungiwe Kombe la Dunia'

Mshambuliaji huyo wa Liverpool alipamba vichwa vya habari wiki hii baada ya picha kuonesha kuwa akimg’ata begani beki wa Italia, Giorgio Chiellini wakati wa mchezo wa Kundi D wa kumaliza hatua ya makundi huku timu yake ya Uruguay ikiibuka na ushindi wa bao 1-0.

Jana jioni, Shirikisho la Soka la Kimataifa lilitangaza kumfungia Suarez mechi tisa za kimataifa, kumfungia kushiriki soka kwa miezi minne na kumtoza faini.

Ataanza kutumikia adhabu katika hatua ya 16 bora. Na Zyryanov alibainisha kwamba iwapo Suarez atafungiwa, basi Fifa inatakiwa kutoa adhabu hiyo baada ya kumalizika kwa fainali za Kombe la Dunia zinazoendela hapa Brazil.

“Ningependa kumuona akicheza mechi zote zilizosalia za kombe la Dunia, kwani kama atapewa adhabu ya kufungiwa inatakiwa iwe baada ya Kombe la Dunia,” alisema katika mahojiano na gazeti la Sport-Express.

“Tayari alikuwa na matukio kama haya, alishamng’ata Branislav Ivanovic na akafungiwa mechi 10.Wanasema kwamba nje ya uwanja Suarez ni mtu mzuri tu, lakini wakati akiwa dimbani hugeuka na kuwa kama mnyama. Lakini nashauri adhabu yake itekelezwe baada ya michuano hii ya Kombe la Dunia.”

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ...

foto
Mwandishi: BRASILIA, Brazil

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi