loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Sumatra kubana mabasi ya mikoani

Hayo yalibainika Dar es Salaam jana wakati mamlaka hiyo ilipofanya ukaguzi wa ghafla wa mabasi na madereva kwa lengo la kuhakikisha sheria zinafuatwa.

Aidha katika ukaguzi huo, kati ya mabasi 200 yaliyokaguliwa, dereva mmoja alibainika kutumia pombe.

Ofisa Mfawidhi wa Sumatra Kanda ya Mashariki, Conrad Shio alisema baada ya ukaguzi huo walibani magari mengi yanaondoa namba ambazo abiria hupaswa kuzitumia kutoa taarifa.

“Kutokana na kuona mabasi mengi hayana, wapo waliodai yamefutika au vioo vilivunjika. Hivyo tumewapa siku ya leo (jana) na kesho (leo) kila gari liwe na orodha hiyo na lisilokuwa nalo tutachukulia hatua,” alisema.

Alisema pia wamebaini kuwa magari ya masafa marefu, yana dereva mmoja badala ya wawili kama inavyoelekezwa na sheria na kuwaagiza madereva na makondakta kufuata sheria wanapoanza safari, ikiwa ni pamoja na kuwa na nyaraka mbalimbali ikiwemo leseni.

Mrakibu wa Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani, Abel Swai alisema ukaguzi wa mara kwa mara umeleta mafanikio kwa madereva wengi kufuata sheria.

Alisema lengo ni kuongeza ufanisi na kupunguza ajali. Alionya madereva watakaokutwa wamelewa watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria inayoelekeza faini ya Sh 50,000 hadi Sh 300,000 .

Kiongozi wa kamati ya utendaji wa chama cha madereva wa kituo hicho, Bonifas Prosper alipongeza ukaguzi huo lakini alitaka kufanyika nchi nzima kwa mara moja.

VIJIJI 73 kati ya vijiji 77 vya Wilaya ya Missenyi ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi