loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Sumaye- Muungano ukivunjika wote tutapoteza

Amesema wako watu wanadhani amani yetu imetua kutoka angani, wengine wanahoji kuwa Muungano ukivunjika kuna madhara gani na kuwataka Watanzania kuwajibu kuwa madhara ni mengi na sisi hatuko tayari kufanya majaribio ya hatari namna hiyo.

Amesema hayo juzi alipozungumza na wananchi katika michezo ya riadha ujirani mwema ya Unguja, Pemba na Dar es Salaam inayofanyika Zanzibar.

“Tumeungana kwa miaka hamsini hivyo kuna mengi ambayo yanahitaji marekebisho na mengine mabadiliko na labda mapya kuingizwa katika makubaliano yetu lakini Muungano wetu tuulinde kama mboni ya jicho letu.

“Nje ya Muungano hakuna manufaa kwa bara wala kwa Zanzibar bali sote kila moja ana la kupoteza. Ndani ya miaka hamsini ya Muungano Watanzania wa pande zote mbili tumeingiliana sana kiasi kwamba si rahisi na wala haiwezekani kututenganisha bila nusu kaputi na baada ya hapo utakuwa umetuachia ulemavu mkubwa,” alisema Sumaye.

Alisema anatambua kuwa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ipo katika hatua mbali mbali za mijadala na katika hali hiyo kuna mambo ya hatari ambayo yamejitokeza. “Jambo la kwanza na ni kubwa ni kuwa tumewaaminisha Watanzania kuwa Katiba mpya ikipatikana, basi ndiyo dawa ya matatizo yetu yote Watanzania kana kwamba matatizo yaliyoko yanatokana na katiba yetu iliyoko.

“Tunawaaminisha Watanzania kuwa Katiba mpya ikipita basi umasikini unatoweka, magonjwa yanatoweka, rushwa na ufisadi vitatoweka, madawa ya kulevya yatatoweka, ujambazi na mauaji yatatoweka na kadha wa kadha.

“Mtizamo huu potofu ni hatari kwa sababu Katiba haitatatua matatizo haya. Matatizo haya yatatatuliwa na Serikali kwa kushirikiana na wananchi wake. Lazima tuwe na Serikali inayoyaona haya matatizo na ikatumia sheria kuyakabili matatizo yanayowasibu raia wake, wananchi lazima wawe tayari kutoa ushirikiano wao kwa serikali yao,” alisema.

Alitaja jambo lingine ambalo limezaliwa katika mijadala hiyo ya Katiba ambalo nalo ni la hatari, kuwa ni kuwaaminisha Watanzania kuwa Muungano wetu ndiyo msingi wa matatizo yetu.

RAIS John Magufuli amewataka wasaidizi wake ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi