loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Sumaye- Wala rushwa wengi matajiri

Aliyasema hayo juzi usiku wakati akihojiwa na kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha ITV. Sumaye amekuwa akikemea vitendo vya rushwa na kusema watu wengi wamekuwa wakisema rushwa inatokana na mishahara midogo.

Hata hivyo alisema wengi wanaojihusisha na rushwa ni matajiri wakubwa wakijaribu kununua haki za wenzao kwa manufaa binafsi.

Alisisitiza kwamba uchafu huo haupaswi kufumbiwa macho kwa kuwa ni adui wa haki, unarudisha nyuma maendeleo ya nchi na pia unakatisha watu tamaa ya kufanya mambo mengi ya maendeleo.

Alisema dawa ya kupambana na rushwa ni kutofumbia macho vitendo hivyo, kwani hakuna asiyejua kwamba rushwa ni kosa na ni dhuluma katika jamii.

Licha ya kuzungumzia rushwa, Sumaye pia alisema anapenda kuona Rais ajaye wa Tanzania anakuwa na ufahamu mkubwa wa jinsi ya kusimamia uchumi ili aweze kuendeleza kazi nzuri ya Rais Jakaya Kikwete anayemaliza muda wake.

“Ahakikishe nguzo kuu za uchumi hazishuki, bali ziwe imara na zisitetereke. Lazima mapato ya serikali kwanza yaongezeke na kubwa zaidi ni kusimamia matumizi ya serikali na yaendane na bajeti ya serikali,” alisema kiongozi huyo mstaafu anayesisitiza pia umuhimu wa elimu, akitaka juhudi zifanyike ili kurejesha ubora uliokuwepo zamani.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amesema serikali imeweza ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi