loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TACAIDS waisifu Tayoa kukabili Ukimwi

Hayo yalisemwa leo na makamishna hao walipotembelea shirika hilo kujionea kazi mbalimbali zinazofanywa na shirika hilo katika kukabiliana na janga la Ukimwi hapa nchini.

Akizungumza kwa niaba ya makamishna wenzake, Diana Chilolo ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), alisema shirika hilo limekuwa likijipanua katika utoaji wa elimu hiyo mwaka hadi mwaka.

“Tutalishauri Bunge tufungue vituo kama hivi angalau kila kanda maana kwa kufanya hivyo tutapunguza maambukizi ya VVU...kuna haja ya kuwapongeza maana mnafanyakazi kwa manufaa ya Watanzania na si kwa manufaa yenu binafsi,” alisema Chilolo.

Kamishna mwingine, Daniel Machemba, alisema alilijua shirika hilo lakini hakuwa anajua kazi kubwa zinazofanywa kwa ajili ya kuelimisha vijana na watu wa rika mbalimbali kuhusu Ukimwi. “

”Awali nilidhani mnajihusisha na uelimishaji Ukimwi kwa kutumia ujumbe wa simu tu kumbe kuna kazi nyingi zinafanyika kama kuhamasisha wanaume kufanya tohara na mambo ya ujasiriamali mnastahili pongezi sana,” alisema Machemba.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Tayoa, Peter Masika alisema shirika hilo kwa kushirikiana na Tacaids wameanzisha kampeni ya kuhamasisha kuzuia kupata maambukizi ya Ukimwi inayowalenga wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu katika muda wote wanapokuwa vyuoni.

Alitaja vyuo vinavyoshiriki kampeni hiyo kuwa ni pamoja na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM),Taasisi ya Uhasibu (TIA), Ustawi wa Jamii, Chuo Kikuu Huria (OUT), Mwalimu Nyerere, Chuo cha Biashara (CBE), Chuo cha Afya Muhimbili na Chuo Kikuu cha Masana kwa upande wa vyuo vya jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wa Mkoa wa Morogoro, Masika alisema vyuo vinavyoshiriki ni pamoja na Chuo Kikuu cha Mzumbe, Sokoine, Jordan ambapo kwa Mkoa wa Dodoma vyuo hivyo ni CBE St John, Chuo Kikuu cha Dodoma na Chuo cha Mipango.

OFISA Masoko wa Halmashauri ya Jiji ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi