loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Taifa kutotumia tiketi za elektroniki

Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Boniface Wambura aliwaeleza waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuwa mfumo huo utaanzia kwenye Uwanja wa Azam Complex na mikoa mingine yote.

Wambura alisema utachelewa kidogo kwenye Uwanja wa Taifa ili kuangalia kwanza mfumo huo unavyofanya kazi katika viwanja vingine.

“Kwa viwanja vinavyotumia mfumo huo tiketi zinanunuliwa kupitia mtandao wa Vodacom ambapo mteja ni lazima awe amesajiliwa katika M-Pesa,” alisema.

Alisema mteja ataanza kwa kupiga *150*03*02# ambapo atapewa namba ya kumbukumbu anayotakiwa kuihifadhi kwani ataulizwa wakati anafanya malipo kwa kupitia M-Pesa ambapo ataingia kama kawaida kwa kutumia *150*00#.

Wambura alifafanua kuwa baada ya kulipa atapewa namba ya tiketi ambapo atakwenda kwenye mashine maalumu za kuchapa (printer) ambazo ziko katika vituo mbalimbali na kuchapa tiketi hiyo ambayo ndiyo atakayokwenda nayo uwanjani.

Alisema njia nyingine ya kununua ni kwa wateja wa Benki ya CRDB ambayo wamejisajili kwenye Sim Banking. Wao wataingia kwa kutumia *150*03# na kufanya malipo ya tiketi. Nao baada ya kupata namba watakwenda kuchapa tiketi kwenye mashine hizo maalumu.

Pia alisema tiketi zinapatikana kupitia maduka ya CRDB Fahari Huduma ambayo yapo katika maeneo mbalimbali nchini.

Watakaonunua katika maduka hayo watapata tiketi na kwenda moja kwa moja uwanjani.

Katika hatua nyingine, TFF imewataka makocha na maofisa habari wa klabu za Ligi Kuu kujiepusha na kauli za chuki, uchochezi na uongo kwa shirikisho na waamuzi pindi zinapofanya vibaya.

Wambura alisema ni muhimu zaidi kuzungumzia matokeo ya timu zao kiufundi badala ya kushambulia waamuzi na TFF kwa maneno makali.

Pia, maofisa habari nao wanatakiwa kuwa makini katika kauli zao kuhusu matokeo na masuala mengine, na kwamba watakaokwenda kinyume, TFF itawafikisha kwenye vyombo vya kinidhamu na maadili kwa ajili ya kuchukuliwa hatua stahiki.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Silas Mwakibinga alitoa onyo kwa mashabiki kutojihusisha na vurugu kwa vile kufanya kutazigharimu timu zao.

Klabu ya Liverpool na Manchester United zipo vitani kumuwinda ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi