loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Taifa Stars kwenda Botswana wiki ijayo

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu kambi hiyo, Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema lengo la kutafuta kambi nje ya nchi ni katika kuhakikisha Stars inajiandaa vizuri ili kufanya vyema.

Wambura alisema benchi la ufundi kwa kushirikiana na uongozi wa TFF ulijadiliana na kupendekeza kutafuta mazingira tulivu yanayoendana na ya nchini kukiandaa kikosi hicho kutimiza malengo yake.

“Uongozi ulijadiliana ukaona uchague Botswana katika mazingira mazuri yanayoendana na ya hapa nchini, kwa hivyo, tunaendelea kuangalia ni wapi watashukia na kuweka kambi yao na wiki ijayo waanze safari yao,” alisema Wambura.

Wambura alisema idadi ya wachezaji watakaoondoka watachaguliwa na Kocha Mkuu Mart Nooij. Kuhusu wachezaji wa kimataifa wa Tanzania wanaocheza TP Mazembe, alisema wataungana na kikosi hicho kama watapewa ridhaa na uongozi wa klabu hiyo wakiwa hawana mechi dhidi ya klabu yao.

Kwa mujibu wa Wambura, mara baada ya kupata mazingira ya kufikia, watataja tarehe ya kuondoka wachezaji hao pamoja idadi kamili ya kikosi kinachotakiwa.

Taifa Stars ikifanikiwa kushindadhidi ya Msumbiji nyumbani na ule wa marudiano, itaingia katika hatua ya makundi ikiwa katika Kundi F lenye timu za Zambia, Cape Verde na Niger.

Katika hatua nyingine, timu ya vijana ya Serengeti itachuana Julai 18, mwaka huu dhidi Afrika Kusini katika mpambano utakaofanyika kwenye Uwanja wa Chamazi Complex, Dar es Salaam.

Wambura alisema katika mchuano huo wa kufuzu mashindano ya Vijana Afrika, Serengeti iliingia moja kwa moja kwenye mzunguko wa pili hivyo, ikifanya vyema katika mchezo wa nyumbani na ule wa marudiano watasonga mbele kwenye mzunguko wa tatu.

“Vijana wote wataanza kufanyiwa vipimo vya MRI kisha kitachaguliwa kikosi ambacho kitaingia kambini kujiandaa na michuano hiyo,” alisema.

TIMU ya Ruvu Shooting imeboresha kikosi ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi