loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Taifa Stars yaaminiwa Msumbiji

Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, ilitua jijini Maputo Ijumaa jioni tayari kwa mechi hii muhimu ambayo Stars inatakiwa kushinda au kupata sare ya kuanzia 3-3. Katika mechi ya kwanza ililazimishwa sare ya mabao 2-2.

Stars walipokewa kwa shangwe na Watanzania wanaoishi Msumbiji huku wakisema wana matumaini na kikosi hiki kinachonolewa na Mart Nooij ambaye aliwahi kuifundisha timu ya Taifa ya Msumbiji.

“Tuna imani sana na kikosi hiki na pia maandalizi yaliyofanyika ni mazuri kutosha kutuletea ushindi,” alisema Anuari Aziz ambaye ni Katibu wa Chama cha Watanzania waishio Msumbiji.

Aziz alisema Msumbiji wenyewe wanaichukulia mechi hii kwa umuhimu mkubwa kwani wameshaona uwezo wa Tanzania na wanajua lolote linaweza kutokea.

“Tumejiandaa vizuri kushangilia maana sisi kama mashabiki ni mchezaji wa 12… tutawashangilia kwa nguvu zote ili tuweze kupata ushindi huu muhimu,” aliongeza Katibu huyo.

Mtanzania mwingine, Salum Ngamba alisema ushindi ni lazima katika mechi hii kwani kikosi ni kizuri na ari ya wachezaji iko juu.

“Tumefuatilia maendeleo ya timu tangu udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager uanze na kwa kweli mambo mengi yamebadilika. Timu sasa inaandaliwa vizuri kwa ushindi kwa sababu kuna uhakika wa mambo mengi kutokana na kuwa na mdhamini wa uhakika,” alisema Ngamba.

Alisema kinachotakiwa kwa mechi hii ni mpira wa kushambulia kuanzia mwanzoni na kwamba Stars idhamirie kufunga mabao ya mapema na kuyalinda kwani uwezo huo upo.

Naye Maalim Ndeta alisema Msumbiji wana wasiwasi mkubwa kwani wanafahamu kuwa Nooij anaifahamu timu yao vizuri na ameuzoea Uwanja wa Zimpeto ambapo mechi hiyo itapigwa.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akizungumza kutoka Dar es Salaam, alisema hii ni mechi muhimu na ushindi ni lazima.

“Sisi kama wadhamini tunategemea ushindi ili thamani ya fedha tulizowekeza iweze kuonekana kwa huu udhamini mkubwa mno wa zaidi ya bilioni mbili za kitanzania kila mwaka,” alisema.

TIMU ya Ruvu Shooting imeboresha kikosi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Maputo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi