loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tamasha la madereva, mafundi magari

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, mmiliki wa Kampuni ya Jossekazi Auto Garage ambaye ni muandaaji wa tamasha hilo alisema tamasha linatarajiwa kufanyika Septemba 27 na 28 katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

Alisema wameamua kufanya tamasha hili ili kuwasaidia wamiliki wa magari kupata huduma hii kwa gharama ndogo ya Sh 20,000 tu kwani imeonekana gharama za huduma za utengenezaji wa magari zinahitaji pesa nyingi.

Aliongeza kuwa huduma hii itatolewa na mafundi wapatao 50 waliobobea katika fani ya ufundi wa magari na wateja watatengenezewa viyoyozi vya magari na kujaziwa gesi, kukaguliwa matairi, betri na kupata ushauri wa kiufundi kuhusu magari yao.

Aidha, alisema katika tamasha hilo wameandaa warsha maalumu kwa akina dada kwani wengi wanaendesha magari kwa sasa na lengo ni kutaka kuwapa uelewa juu ya ni nini cha kufanya pindi wanapopata na hitilafu kwenye magari yao barabarani.

“Akinadada wengi wamekuwa wakikutana na changamoto za kuharibikiwa magari wakati mwingine kwenye dashibodi ya gari kunakuwa na alama za hatari lakini wanawake wengi wamekuwa wakipuuzia alama hizo na matokeo yake wanasababisha hasara kubwa,” alisema.

Mkurugenzi wa Jast Tanzania Limited, Jahu Kessy ambaye ni Mratibu wa tamasha hilo alisema kila kitu kinaenda vizuri. Alisema baada ya tamasha hilo mafundi hao watatembelea Hospitali ya CCBRT kusaidia akinamama wenye matatizo ya fistula.

WIZARA ya Habari, Utamaduni, Sanaa na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi