loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tanzania hupoteza hekta 400,000 za misitu kila mwaka

Katika swali la Kilango alitaka kufahamu athari ambazo taifa linapata kutokana na kuzalisha mkaa kwamba Tanzania inazalisha tani milioni moja za mkaa kwa mwaka na asilimia 50, ya mkaa huo hutumika Dar es Salaam.

Kitwanga alisema kwa kiasi kikubwa misitu hiyo hupotea kutokana na shughuli za ukataji miti kwa ajili ya kutengeneza mkaa na kuni.

“Takwimu zinaonesha asilimia 90, ya matumizi ya nishati nchini inapatikana kutoka kwenye kuni na mkaa ambapo mkaa hutumika mijini kama Dar es Salaam na kuni hutumika vijijini,” alisema Kitwanga.

Alisema athari za kuzalisha mkaa kwa wingi ni pamoja na kusababisha mmomonyoko wa udongo, kupungua kwa malisho, kupungua kwa mvua, ongezeko la hewa ukaa na uharibifu wa bionuwai ambapo wanyama na baadhi ya mimea vinatoweka.

Alisema suala la Dar es Salaam kutumia nishati ya umeme badala ya mkaa linaweza likawa sahihi kwa watu wachache kwa kuwa gharama za umeme ni kubwa.

Alisema pia kwa sasa mtandao wa nishati ya umeme nchini bado ni mdogo ambao ni asilimia 20, tu ya watanzania ndio waliofikiwa na nishati hiyo.

“Serikali inaendelea kuhimiza wananchi kutumia nishati mbadala kama gesi ya kupikia, majiko banifu na majiko yanayotumia nguvu za jua hususan kwa wakazi wa mijini", alisema Kitwanga.

BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imepongeza uthubutu ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi