loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tanzania, Kenya zatoshana nguvu michuano ya Majeshi

Tanzania ambayo ilikuwa tayari imeshakubali matokeo ilifanikiwa kusawazisha bao hilo katika dakika za nyongeza.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa na upinzani mkali mwamuzi huyo aliongeza dakika nne ambazo zilitoa nafuu kwa Tanzania ambao walipata bao hilo la kusawazisha kupitia kwa nahodha wao, George Minja.

Kenya walitangulia kupata bao lao kupitia kwa mchezaji wao Sylus Shitote katika dakika ya 62. Timu zote hizo sasa zimebakiwa na mchezo mmoja ambapo kufuatia matokeo hayo kila moja inaweza kufikisha pointi saba na kubakisha kitendawili kikubwa cha nani kuwa bingwa katika soka.

Katika mechi nyingine iliyochezwa juzi, Uganda ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Rwanda, mabao ya Uganda yalifungwa na Watende Ezekiel dakika ya 33 na Muteb Shalif dakika ya 84 wakati la Rwanda likifungwa na Iradukunda Betrand dakika ya 32.

Kwa upande wa mchezo wa kikapu, timu ya Uganda ilishinda dhidi ya Burundi vikapu 59-52 katika mchezo wa michuano hiyo uliochezwa uwanja wa Gymkhana mjini hapa.

Aidha Netiboli wanawake, Uganda iliibuka na ushindi wa mabao 94-5 dhidi ya Burundi katika mchezo uliochezwa uwanja wa JKU Saateni.

MKOA wa Pwani umeanza kwa kishindo maandalizi ya kushiriki mashindano ...

foto
Mwandishi: Mwajuma Juma, Zanzibar

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi