loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Tanzania yalaani mauaji ya Wapalestina

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, John Haule jana ilisema Serikali ya Tabzania inaomba Jumuiya ya Kimataifa kuendelea kuunga mkono juhudi za Kidiplomasia za kumaliza mgogoro huo kwa amani.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Julai 14, Mwaka huu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kwa niaba ya serikali ya Tanzania aliimba Israel na Hamas kusitisha mapigano na kuomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuingilia kati krudsiha amani Mashariki ya Kati.

Taarifa hiyo iliendelea kusema kiini cha ufumbuzi wa mgogoro huo ni kuwapa watu wa Palestina haki ya kujitawala kuanzisha Taifa Huru la Palestina.

Ilisema serikali ya Tanzania itaendelea kuunga mkono suluhu itakayopatikana kwa ushirikiano wa pande zote mbili za Palestina na Israeli kwa amani na kuhakikisha usalama wa Taifa la Israeli.

MAFUNDI umeme nchini wametakiwa kufanya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi