loader
Picha

Tanzania yatetea ubingwa michuano ya Majeshi

Tanzania ambayo ilikuwa mwiba mkali kwa mchezo huo ilitwaa ubingwa huo kwa kuifunga Uganda mabao 32-30.

Mwaka jana walipokutana waliwafunga mabao 38-32. Katika mchezo huo, Tanzania iliwatumia wafungaji wake Mwanaidi Hassan ambaye alifunga magoli yote 32 akishirikiana vizuri na Faraja Malaki.

Kwa upande wa Uganda ambao wamekuwa wateja wakuu wa Tanzania waliwatumia wafungaji wake Makiwu Annet aliyefunga magoli 18 na Allupo Caro (GA) aliyefunga mabao 12.

Mbali na mchezo huo pia kulifanyika mchezo kati ya Kenya na Rwanda ambapo Kenya ilishinda kwa magoli 75-5 hivyo kushika nafasi ya tatu.

Kwa mchezo wa mpira wa mikono timu ya Tanzania imeshinda kwa mabao 29-19 dhidi ya timu ya Rwanda wakati Kenya iliifunga Burundi kwa ushindi mwembamba wa mabao 31-29.

Aidha kwa upande wa mpira wa Kikapu Tanzania imefungwa na Uganda mabao 59-59 na Rwanda kufungwa na Kenya mabao 59-34.

KLABU ya Simba imeiomba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, ...

foto
Mwandishi: Mwajuma Juma, Zanzibar

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi