loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Taratibu za upigaji kura Tamasha la Pasaka hadharani

Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Abihudi Mang’era, kazi hiyo ya upigaji kura itahusika kuchagua mikoa, mgeni rasmi na waimbaji watakaoimba katika tamasha hilo.

Mang’era alisema mwaka huu wametoa nafasi hiyo ili kuwapa nafasi mashabiki wa muziki wa Injili kuchagua mikoa, mgeni rasmi na waimbaji watakaoshiriki.

Alifafanua kuwa ili kumchagua mgeni rasmi, unaanza na neno Pasaka unaacha nafasi kisha jina la mgeni rasmi kwenda namba 15327 katika simu za mkononi.

Mang’era alisema kumchagua mwimbaji katika tamasha hilo ni kuandika neno Pasaka, unaacha nafasi jina la mwimbaji kwenda namba 15327 wakati kuchagua mkoa, unaandika neno Pasaka, unaacha nafasi kwenda namba 15327.

Makamu Mwenyekiti huyo alitoa mwito kwa Watanzania kupiga kura kuchagua nafasi hizo tatu ili kufanikisha tamasha hilo la kila mwaka linaloandaliwa na Kampuni ya Msama Promotions.

KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi