loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tathmini ya kina kufanywa kuhusu tiketi za elektroniki

Uamuzi wa kusitisha tiketi hizo umetokana na kikao cha Sekretarieti ya TFF na Benki ya CRDB kilichokaa juzi kujadili changamoto zilizojitokeza kwa muda mfupi tangu kuanza kwa utumiaji huo kwenye viwanja mbalimbali vinavyotumika kwa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Boniface Wambura alisema jana kuwa tangu kuanza kutumika kwa mfumo huo, kumekuwa na changamoto zikiwamo za msongamano wa watu, watu wawili kutumia tiketi moja kutokana na ufinyu wa elimu na mashine kushindwa kufanya kazi vizuri kutokana na kuzidiwa.

Pamoja na hizo, baadhi ya watu walikuwa wakilalamika uchache wa mashine kwenye uwanja mmoja, wakitolea mfano CCM Mkwakwani Tanga ambapo katika mechi kati ya Coastal Union dhidi ya Yanga, kulikuwa na msongamano kutokana na uchache wa mashine zenyewe kutofungwa katika milango yote.

“Sio kila mtu anapenda utumiaji wa tiketi hizo, wapo baadhi ya watu wanataka kuona tunashindwa, hiyo pia ni changamoto, lakini muda sio mrefu tutatangaza tena utumiaji huo baada ya tathmini,” Wambura aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana.

Alisema sababu nyingine ya kusitisha tiketi hizo, ni hadhari iliyotolewa na vyombo vya Usalama juu ya misongamano inayotokea uwanjani kutokana na kutokuwepo mtiririko mzuri wa uingiaji. “Tayari zipo changamoto

TIMU ya Ruvu Shooting imeboresha kikosi ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi