loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TAZARA yapewa wiki moja kulipa mishahara ya miezi 5

Mukoba alisema hayo jana, Dar es Salaam na kuongeza kuwa wafanyakazi wa Tazara upande wa Tanzania, hawajalipwa mshahara wao tangu Aprili mwaka huu, hali inayowafanya waishi maisha magumu.

Alisema alichaguliwa mwezi uliopita Dodoma na alikabidhiwa baadhi ya matatizo ya wafanyakazi na suala la kutolipwa wafanyakazi hao likawa na uzito wa kipekee.

Mukoba alisema alianza kujielimisha kuhusu mgogoro huo kwa kuwa jirani na viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli (TRAWU).

“Taarifa nilizonazo ni kwamba Serikali imetoa pesa inayotosha mishahara yao ya miezi minne na pesa hiyo iko kwenye Mamlaka ya Tazara.

“Hivyo nawataka viongozi wa Tazara kukamilisha taratibu za malipo hayo kurejesha utu wa wafanyakazi hao,” alisema Mukoba.

Alisema zaidi ya kuvunja haki za kiraia na haki za wafanyakazi kunakofanywa na mamlaka hiyo bado viongozi wa Serikali wamesikika wakitoa vitisho vya kuwafukuza kazi wafanyakazi watakaogoma.

“Mtume alisema mwajiri amlie mfanyakazi ujira wake kabla jasho lake halijakauka….. sasa miezi mitano imepita hilo jasho halijakauka kweli,” alihoji Mukoba.

Alisema mateso waliyopata wafanyakazi hao wa Tazara, yamewasononesha na ni jambo linaloshusha moyo na hamasa kwa wafanyakazi hao kuongeza bidii ya kazi.

“Nawataka wawalipe wafanyakazi hawa ndani ya wiki moja ukiritimba wowote utakaopewa nafasi baada ya pesa kupatikana utatufanya tuelewe kuwa nia ya kuishi na kufanyakazi kwa amani haipo,” alisema Mukoba.

BODI ya Korosho nchini (CBT) imesema taarifa zinazogaa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi