loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TBL kuwezesha wakulima kujitosheleza malighafi

Mkurugenzi wa Kampuni ya TBL Tanzania, Roberto Jarrin alisema hayo kwenye warsha wa wahariri wa vyombo vya habari nchini iliyofanyika kwenye kiwanda cha bia cha jijini Mbeya.

Alisema asilimia 60 ya malighafi zinazotumika kutengeneza bidhaa zinazozalishwa na Kampuni hiyo zinanunuliwa kwa wakulima nchini Tanzania, hali inayosaidia wananchi wanaolima mazao yatumiwa na kampuni hiyo kuwa na soko la uhakika.

Alisema kuwa kampuni hiyo ina viwanda vya bia katika miji ya Dar es Salaam, Arusha, Moshi, Kilimanjaro, Mbeya na Mwanza ambavyo vinahitaji mazao mengi kama malighafi za kutengenezea bidhaa zake.

“Hivi sasa tunanunua mazao ya wakulima wa Tanzania ambao wanatuwezesha kupata asilimia 56 ya malighafi tunazozihitaji kwa jili ya kutengeneza bidhaa zetu, lakini lengo letu ni kuwawezesha wakulima watupatie angalao asilimia 75 ya malighafi tunazozihitaji kwa ajili ya matumizi ya viwanda vyetu,” alisema Jarrin.

Meneja wa Kiwanda cha Bia cha Mbeya, Waziri Jemedari aliyataja mazao yananunuliwa na Kampuni hiyo kama malighafi ya kutengeneza bidhaa zake kuwa ni mahindi, mtama, ngano na shayiri ambayo yote yanapatikana nchini.

Alisema kuwa ikiwa wakulima wataongeza uzalishaji, watasaidia kampuni hiyo kupunguza gharama za uzalishaji kwa kununua malighafi kutoka ndani ya nchi badala ya kuagiza kutoka nje za nje.

Akizungumzia changamoto zinazokikabili kiwanda cha bia cha Mbeya, Jemedari alisema kuwa suala la kutokuwa na umeme wa uhakika wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kwa kuwa umeme unapokatika hulazimika kutumia umeme wa jenereta ambao ni ghali zaidi kuliko ule wa Tanesco.

Katibu wa Jukwaa la Wahiriri ambaye pia ni Mhariri Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena alisema kuwa Serikali ndiyo inayoratibu masuala yote ya uwekezaji nchini, hivyo pia yenye wajibu wa kuhakikisha wawekezaji hao wanapata mahitaji yote muhimu ikiwemo malighafi kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa zao.

Naye, Mhariri wa Gazeti la Uhuru, Joseph Kulangwa aliipongeza Kampuni ya TBL kwa kununua mazao na kuwapatia wakulima soko la uhakika la mazao yao, lakini akaitaka Serikali kuwawezesha zaidi wakulima ili wazalishe zaidi kukidhi mahitaji ya kiwanda hicho.

“Nadhani wakulima wanahitaji kuwezeshwa zaidi katika masuala ya pembejeo, utaalamu na zana bora za kilimo ili wazalishe zaidi kukidhi mahitaji ya viwanda vya ndani, siyo hiki tu bali na vingine vinavyohitaji,” alisema Kulangwa.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi