loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TBS: Usighushi nembo ya ubora ili biashara yako ikue

Anasema, biashara inahitajika kwa sababu ni moja ya shughuli zinazochangia kujenga uchumi wa mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla. Lakini, anaonya kuwa, si kila biashara inaweza kuujenga uchumi, hasa pale inapotokea kwamba mfanyabiashara husika anapuuza sheria za uzalishaji, zinazomtaka azalishe bidhaa zenye viwango vya ubora vilivyopitishwa na TBS.

Kwa maelezo yake, kuna uhusiano kati ya biashara zisizo na ubora na kuporomoka kwa uchumi. Anasema, uhusiano wa kwanza ni pale wateja wanapobaini kuwa bidhaa wanayoifuata ili kuinunua haifai kwa matumizi, hivyo kutoinunua. Pili, uhusiano mwingine anasema hutokea pale mtumiaji au mnunuzi anaponunua bidhaa hafifu, kuitumia na kupata madhara ya moja kwa moja mwilini.

Kwa mfano vyakula visivyo na viwango vya ubora uliopitishwa na TBS, hata kama vina nembo isiyo ya halali ya shirika hilo. Madhara mengine ya moja kwa moja yanatokana na matumizi ya vipodozi, vifaa vya vyombo vya moto vinavyoweza kusababisha ajali kwa kukosa viwango vya ubora, vifaa vya ujenzi kama vile nondo na matofali na vingine vinavyotambuliwa kuwa katika kundi la bidhaa zinazoweza kuleta madhara ya moja kwa moja kwa mtumiaji endapo vitakuwa na ubora hafifu.

“Nembo ya TBS si alama inayofichwa ili umma isiifahamu. Inatangazwa kwenye vyombo vya habari na mara kwa mara tumekuwa na semina zinazohusisha wadau wa biashara ya bidhaa mbalimbali, wakiwemo wazalishaji wa ndani wanaopewa fursa ya kuifahamu kwa kuoneshwa namna inavyofanana pamoja na kuelekezwa tofauti yake na alama hiyo iliyoghushiwa,” anasema.

Kutokana na maelezo yake, anayetumia alama isiyo ya TBS kwa kulazimisha mfanano anatafuta mwenyewe kufa kibiashara, kwa sababu, anaifahamu wazi hatari inayoweza kumpata pindi anapokamatwa na maofisa wa shirika akiitumia.

“Kutoza faini ni moja ya adhabu anayopewa mfanyabiashara anayeghushi nembo yetu, kwa sababu ya kuwauzia wateja bidhaa asizopaswa kuwauzia. Lakini, adhabu nyingine anayoweza kupewa ni kuzuiwa kuendelea na biashara, pamoja na kufikishwa mahakamani na kufungwa,” Mwanasheria huyo anaeleza na kufafanua kuwa kuzuiwa kufanya biashara ndio kujiua kibiashara.

Mbali na hayo, anasema, biashara yoyote inayoingia kwenye midomo ya watu na kuzungumzwa kwa ubaya kutokana na madhara iliyowasababishia watumiaji huwa vigumu kukua kwa sababu wateja hupeana taarifa mbaya kama wanavyopeana zilivyo nzuri na hivyo kuzikataa zifikishwapo sokoni.

“Ukishaona biashara yako hainunuliwi ni lazima ujiulize, je, ubora wake unafaa? Vile vile, una wajibu wa kujiuliza endapo haifai ni wapi umekosea ili urekebishe. Endapo utakaza shingo na kuzuia taarifa za wateja sokoni zisibadilishe aina ya uzalishaji wako na ubora wa bidhaa, hutaweza kukua kibiashara na hata kutangaza biashara hiyo kwenye vyombo vya habari kutakuwa ni kupoteza fedha bure,” anasema.

Anasema endapo mafanikio ya mwanzo yatamlewesha mfanyabiashara na kuendelea kufanya biashara yake bila kuzingatia sheria za viwango, eti kwa sababu wapo wanaonunua bidhaa anazozalisha, atadumaa kibiashara kwa sababu siku za kuiendesha kwa uwazi zitakwisha kutokana na kusakwa na shirika, hatimaye kuifunga mwenyewe au kupoteza wateja wa msingi.

Wateja na bidhaa hafifu Inaelezwa kuwa wateja wengi hasa katika maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu hukimbilia bidhaa zinazoingia sokoni kwa mara ya kwanza, hivyo kukosa nafasi ya kuchunguza endapo zina ubora uliopitishwa na shirika au la.

Kadhalika, Bitaho anaweka bayana kuwa, baadhi ya wateja huzifuata, licha kuambiwa kuwa hazifai kwa matumizi kwa sababu ni hafifu, kwa kuwa bei ya bidhaa hiyo huwa ni ya chini kuliko ilivyotarajiwa, na wanakuwa vipofu wa madhara yanayoweza kuwapata kiafya ama mengine baada ya kuzitumia.

“Tumejionea na ninyi mmejionea kwamba wateja wananunua vyakula au vifaa na kudai kuwa vimewadhuru. Tunapovifanyia uchunguzi katika maabara zetu za kisasa tunagundua kuwa vyakula hivyo, au vifaa hivyo havina ubora unaotakiwa”. “Bidhaa nyingine hutengenezwa nyumbani kiholela bila TBS kuwa na taarifa ya kuwepo utengenezaji au uzalishaji huo katika eneo husika. Matokeo yake, uzalishaji huo holela huendelea kwa muda hadi tunapobaini uwepo wa mzalishaji holela tayari watumiaji huwa wameshadhurika,” anasema.

Wajibu wa mteja Mteja yeyote yule, mkubwa au mdogo, wa kudumu au wa muda, ana wajibu wa kutoa taarifa katika shirika la viwango (TBS) endapo atabaini uwepo sokoni wa bidhaa halali zisizo na ubora, ili shirika lifanye utaratibu unaostahili kuziondoa. “Tumefanya hivyo kwenye viwanda vinavyotengeneza achali za nyanya, sabuni, nondo na nyinginezo na tumekuwa katika shughuli endelevu ya kuondoa sokoni nguo za ndani za mitumba katika mikoa mbalimbali ya Tanzania,” anasema.

Mwanasheria huyo anaendelea: “Kutokana na hilo, hatusiti kufanyia kazi taarifa zozote za kuwepo uzalishaji batili wa bidhaa zinazoweza kumwathiri mteja moja kwa moja, hivyo umma utujulishe kinachoendelea tufanyie kazi. Tunapenda kujulishwa alipo mzalishaji asiyefuata maelekezo yetu na hasa anayeghushi nembo yetu.”

Anasema kuwa lengo la kuwafuatilia wazalishaji wa aina hiyo si kuwaadhibu tu, bali kuwaelimisha umuhimu wa kuzalisha bidhaa zenye viwango vya ubora vinavyotakiwa.

“Tunawachukulia hatua za juu baada ya kuwaonya na kuwapa elimu kuhusu uzalishaji unaozingatia viwango, hivyo jamii isiwafiche wazalishaji wasio na nembo za TBS ama wanaozighushi ili kuficha uhafifu wa bidhaa zao kwa kuwa kuwalinda huko hakuna faida kwao wala kwa taifa,” anasema.

Kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa ...

foto
Mwandishi: Namsembaeli Mduma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi