loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

‘Tehama itaimarisha biashara za mipakani’

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye alisema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Alisema hayo katika warsha ya kujadili ripoti ya Mshauri Mwelekezi kuhusu fursa za kuongeza uwazi na kupambana na rushwa kwenye biashara za mipakani katika mwendelezo wa tafiti zilizofanywa na sekta yao kuimarisha mazingira ya biashara nchini.

“Baadhi ya taasisi hapa nchini zina mifumo hii ukiwemo ule wa Tanzania Customs Integrated System (Tancis) na ule wa NTBs SMS and Reporting System lakini hakuna utaratibu unaoiwezesha taasisi zingine kuitumia hasa zile za masuala ya biashara,” alisema Simbeye mwishoni mwa wiki.

Alisema mifumo hiyo inawezesha kuweka sheria na taratibu zote za kibiashara watu waione kwa uwazi zaidi na pia husaidia kufanya mawasiliano yanayolenga kuondoa urasimu na mianya ya rushwa kwa kutoa taarifa kwa vyombo husika.

Akitoa mfano alisema Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) kimeweka mfumo wa kutoa taarifa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno kutoa taarifa mbalimbali zikiwemo za vitendo vya rushwa kwa vyombo kama polisi.

“Matokeo ya utafiti huu yatasaidia kutekeleza Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN),” alisema.

Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi, alisema mifumo hiyo ina fursa kubwa katika kuleta mabadiliko katika utendaji kazi.

“Serikali inatambua mchango wa Sekta Binafsi katika uchumi na utoaji ajira na jitihada zinazofanyika ni kuhakikisha mifumo hii inafanya kazi kwa ajili ya kukuza biashara mipakani,” alisema.

Mtoa mada katika warsha hiyo, John Kyaruzi kutoka Kampuni ya Gotham International alisema baadhi ya taasisi zina mifumo hiyo lakini hakuna uratibu wa kuhakikisha inatumiwa na taasisi nyingine.

Msimamizi wa utafiti huo, Donath Olomi alisema licha ya baadhi ya taasisi kuwa na mifumo hiyo ambayo ina uwezo mkubwa wa kutumiwa na taasisi nyingine, lakini bado taasisi zingine zinataka kununua mifumo mingine licha ya gharama yake kuwa kubwa.

“Mifumo hii kuinunua ni gharama sana, mfumo mmoja unagharimu dola za Kimarekani milioni 50 sawa na Sh bilioni 70 za kitanzania,”alisema na kuongeza kuwa hakuna sababu ya taasisi nyingine kununua kwa vile mifumo iliyopo inaweza kuunganishwa na kutumika kwa shughuli mbalimbali na wengine.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi