loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tengeru kuwa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii

Alisema chuo hicho kilianzishwa mwaka 1963, kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa maofisa maendeleo ya jamii wa kuhamasisha wananchi kujiletea maendeleo.

Mwaka 1983 chuo hicho kilianza kutoa mafunzo ya Stashahada ya Juu katika fani ya maendeleo ya jamii na kimeendelea kupanua wigo wa utoaji mafunzo katika fani mbalimbali, zikiwemo jinsia na maendeleo na upangaji na uendeshaji shirikishi wa miradi.

Alisema mwaka 2008 chuo hicho kilisajiliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ili kutoa mafunzo ya Shahada ya Maendeleo ya Jamii.

Aidha, mwaka 2012 chuo kilianza kutoa mafunzo ya Stashahada ya Uzamili katika fani ya maendeleo ya jamii. Kwa sasa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru kinatoa mafunzo ya Shahada na Stashahada ya Uzamili katika fani ya maendeleo ya jamii.

“Lengo la Azimio hili ni kubadili chuo ili kukiwezesha kujitegemea kiutendaji na kukipa uwezo zaidi wa kujisimamia katika kupanga na kufanya maamuzi yake katika azma ya kupanua na kuboresha utoaji wa mafunzo katika fani za maendeleo ya jamii,” alisema Mhagama.

Kwa upande wake, Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, ilisema inaunga mkono Azimio hilo la kukifanya chuo hicho cha Tengeru kujitegemea.

“Kambi rasmi ya upinzani haipingani na azimio hili, ila kutokana na hali ya chuo ilivyokuwa kwa miaka mingi, inauliza ni kwa nini Azimio hili limechelewa, kwani chuo hiki tayari kingekuwa kinatoa wataalamu wengi,” alisema Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Rajab Mbarouk Mohamed.

Hata hivyo, Rajab alitaja mambo muhimu ambayo serikali inatakiwa kuyashughulikia haraka katika chuo hicho cha Tengeru kuwa ni: madarasa, mabweni, karakana za kujifunzia, uwezo wa chuo kudahili wanafunzi na uwezo wa kitaaluma kwa timu nzima ya wakufunzi, hasa wenye shahada za uzamili na uzamivu.

“Kambi ya upinzani inapongeza uongozi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru kwa jitihada zao za kukiongoza chuo kwa umahiri mkubwa hadi kufikisha katika hatua ya kujitegemea,” alisema Rajab.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto ...

foto
Mwandishi: Nelson Goima, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi