loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TFDA wafunga kiwanda cha mikate

Kufungwa kwa kiwanda hicho kunafuatia ukaguzi wa kushtukiza uliofanywa na maofisa wa TFDA katika taasisi, idara, vituo na viwanda vinavyotoa huduma ya vyakula vinywaji na dawa katika Manispaa ya Kigoma Ujiji vikiendeshwa kinyume na sheria namba moja ya mwaka 2003 ya vyakula na vipodozi.

Akizungumza Mkaguzi wa TFDA Kanda ya Kati, Engelbert Bilashoboka alisema kuwa kufanyika kwa ukaguzi huo wa mara kwa mara kuna lengo la kuwalinda walaji dhidi ya bidhaa zinazozalishwa katika mazingira ambayo yanaweza kuleta madhara kwa jamii.

Mkaguzi huyo alisema kuwa kiwanda hicho cha mikate kimefungwa baada ya kubainika kuwa kinazalisha bidhaa hiyo katika hali ya uchafu huku mikate ikiwa imechanganywa mahali pamoja na viatu, nguo na vitu mbalimbali ambavyo havistahili kuwepo eneo la uzalishaji.

Pamoja na kufungwa kwa kiwanda na kusimamisha uzalishaji hadi marekebisho yatakapofanyika pia TFDA imetangaza kuteketezwa kwa shehena ya mikate iliyokutwa kiwandani hapo ambapo mmiliki atalazimika kulipia gharama za kuteketezwa kwa mikate hiyo.

Kwa upande wake mmiliki wa kiwanda hicho, Gulashan Issa Vislam amewalaumu wasimamizi wa kiwanda kwa kushindwa kutimiza majukumu yao hali inayofanya kiwanda kufanya shughuli zake katika mazingira ya uchafu.

RAIS John Magufuli amewataka wasaidizi wake ...

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah,Kigoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi