loader
Dstv Habarileo  Mobile
THE GIL GLADDER: Chupuchupu imtoe roho Baby Madaha

THE GIL GLADDER: Chupuchupu imtoe roho Baby Madaha

Hii ilijitokeza katika baadhi ya filamu kama Cyborg ya Jean Claude Van Damme alipomtoboa mtu jicho katika harakati za kuigiza. Au Sanj Datty alipoua kwa bahati mbaya wakati akiigiza. Kwa hiyo ajali yoyote yanaweza kutokea, ingawa kwetu ni tofauti sana kwa kuwa watu wanaigiza zaidi kuliko uhalisi wa kitu wanachokiigizia.

Lakini tofauti na filamu ya The Gil Gladder iliyochezwa Kenya na mwigizaji Baby Joseph Madaha ambaye pia alikuwa mshiriki wa Tamasha la Bongo Star Search, pale aliponusurika kuuawa na hata kubakwa. Akizungumza na mwandishi wa makala haya, alisema ni tofauti na uigizaji wa Kitanzania, kwani amegundua mara nyingi unapotafuta uhalisi wa jambo, basi tarajia matukio ya hatari kujitokeza.

Baby Madaha alisema wakati akiigiza filamu hiyo, ambayo inatarajia kutoka mwezi huu, alikutana na mambo mengi ambayo mengine yalifanya maisha yake kuwa hatarini. “Nikiwa nyumbani Tanzania, nimeigiza filamu nyingi, lakini sikuwahi kuona na kuingia matatizoni kama ilivyokuwa kwa filamu hii,” anasema Baby Madaha ambaye pia ni mwimbaji.

Alielezea zaidi kwamba filamu hiyo, ilikuwa ikihusu juu ya matukio ya vijana waishio mitaani, kwa nchini Kenya wanajulikana zaidi kwa jina la chokoraa. Vijana ambao wamekumbwa na mikasa mingi ambayo hatimaye wamejikuta wakiwa na roho ya kijana na kufanya mauaji mengi.

Anasema kutokana na kisa hicho, ikabidi filamu hiyo iigize sehemu halisi ya matukio hayo, kwa kuwa tayari walishafanya uchunguzi na kugundua ni sehemu gani zaidi ambazo inaweza kuwa halisi. Kwa kuwa Meneja wa Kampuni ya Candy n Candy, Joe Kariuki ambaye ndiye mmiliki wa filamu hiyo, ni mtu wa Kenya, hawakuwa na wasiwasi juu ya usalama wao.

Anasema tukio la kwanza ambalo liliwakumba, walienda kuigiza kwenye majumba ambayo watoto wa mtaani wamekuwa wakiishi mara kwa mara. Lakini kumbe wakati wakiigiza katika eneo moja la mtaa, kwa upande wa pili wa mtaa huo huo, yalitokea mauaji ya kweli, ya mtu raia wa Kichina.

Anasema mauaji hayo yaliwafanya wasitishe tukio la kuigiza kwa muda fulani, kwa kuwa wao walikuja kuyashitukia wakati tayari yameshatokea. “Chokoraa wa Kenya au majambazi wa huko, kila kitu wanafanya kimya kimya. Unaweza ukawa nje na ndani watu wakawa wanafanya unyama bila ya wewe kujua,” alielezea Madaha.

Baada ya kuisha kumbukumbu ya tukio hilo, anasema likaja tukio lingine ambalo alikusanya watoto wa Kenya ambao ilipaswa waigize kama watoto wa mtaani ambao pia ni wahalifu. Kwa kuwa Madaha, aliigiza kama kiongozi wa watoto wa mtaani, ilibidi waigie katika makazi ya chokoraa wa ukweli ili wapate kuigiza kipande hicho.

Anasema ilibidi yeye aonekane kama vile anatoa amri kwa watoto hao, waingie mtaani na kuvamia watu na baadaye kumletea kile ambacho wamekipata. Lakini bila kujua kama makazi waliyoingia chokoraa wa kweli walikuwepo, ambao ndiyo sehemu zao za kujificha wanapofanya uhalifu.

Kitendo cha wao kuingia eneo hilo, walijikuta ghafla wamevamiwa na chokoraa hao wa kweli, wakiwa wameshika silaha kama mapanga na vitu vingine.

“Bosi wangu Jor, alikuwa na dola mia nane zote walichukua. Mimi nikapigwa sana, hadi nikavimba jicho. Wakati huo cameraman, alikuwa amekimbia na kujificha kwenye mtaro ili kuhofia kuchukuliwa kamera yake,” anaelezea na kuongeza kuwa wale watoto ambao wao walikuwa wakiigiza kama chokoraa, nao walikula kipigo cha nguvu kiasi cha kukimbia kila mmoja na njia yake.

“Ilikuwa nusura sana kwani kipigo tulichopigwa kilikuwa kikubwa. Nashukuru Mungu hawajatufanyia uhalifu mwingine maana wangeweza hata kutuchoma kisu,” anasema msanii huyo. Baada ya tukio hilo, anasema tukio lingine ambalo nalo lilikuwa hatari wakati wanaigiza filamu hiyo, lilikuwa la kuigiza akimgonga mtu.

Tukio hilo lilimpasa yule ambaye anaigiza akigongwa, ilimbidi alirukie gari wakati linapokuja, jambo ambalo walifanikiwa kufanya hivyo kwa mara ya kwanza. Lakini tukio hilo lilibidi lirudiwe kwa mra ya pili, ndipo balaa lilipoibuka.

“Kwa mara ya pili, nilikanyaga mafuta na kumfuata yule mtu. Lakini sijui ibilisi gani alinipitia mbele yake, kwani gari ghafla breki ziligoma. Na yule mtu bila kujua kama breki ziligoma, alizidi kusimama mbele na alipolirukia, alijikuta nikimgonga kweli,” anafafanua Baby Madaha. Hakuna aliyeamini kama angepona, kwani alirushwa hadi mtaroni na kuzimia papo hapo, hali iliyobidi wamkimbizie hospitali kwa ajili ya huduma ya kwanza.

“Hadi leo ukienda kwa Kenya, na kuwaambia watu waigize na mimi nishike kisu au ajali, wanakataa wanajua sina masihara,” anaongeza. Lakini anasema s i k u moja k u l i - kuwa n a t u k i o lingine ambalo l i l i b i d i w a i g i z e kama vile anashikwa makalio na wateja wa baa, lakini baadaye wanamvuta chooni na kumbaka kwa nguvu.

Kabla ya kuigiza tukio hilo, anasema ilibidi wapumzike baada ya kazi zingine kumalizika. Lakini wakati wakipumzika, wale waliokuwa wakiigiza kumbaka, ilibidi waanze kunywa zile pombe za kuigizia. Hadi muda wa kuigiza ulipofika, walikuwa tayari walishalewa kweli, lakini watu hawakujua kama walikuwa wamelewa sana.

“Nilikuwa naigiza kama mhudumu na kuwaletea vinywaji. Ndipo nikashikwa makalio, lakini kushikwa kwake ilikuwa tofauti na k u l e kuigiza. Nilishituka, lakini nikanyamaza, lakini kasheshe ikaja pale katika kubaka n d i p o h a l i ilipobadilika ghafla,” anaendelea kusema. Waigizaji hao ambao raia wa Kenya, walianza kumgombania kwa nguvu, na ndipo hapo Baby alipojikuta akipoteza nguvu za kweli, maana vidume vya watu walikuwa na uroho wa kweli.

Waliokuwa wakiangalia walijua kazi inaenda vizuri, lakini wakaja kushituka baada ya kuona nguo zikianza kuchanwa, huku watu wakiwa na lengo la kubaka kweli. “Walijitahidi kusimamishwa lakini, walikuwa bado wamepania kunibaka kweli. Ndipo watu wakaamua kuingilia kati na kuanza kuamulia ili kunitoa,” anasema.

Baada ya kutolewa ndipo nguo zao zilipoonesha lengo lao, na hata kusimama vizuri walishindwa kwani walikuwa wakinesa sana. Lakini tukio la mwisho lilikuwa pale alipotekwa na mtu aliyemfanyia unyama. Ilibidi mtu huyo amtese kwa kumtumbukiza kwenye maji.

“Alinitumbukiza kwenye maji mara moja, lakini hatimaye alinikandamizi moja kwa moja na nikaanza kupoteza pumzi na kunywa maji. Watu walikuwa wakiangalia kupitia televisheni dogo ambayo ilikuwa ndani ya maji ndio waliweza kushituka baada ya kuniona natapatapa,” anasema.

Ndipo walipomwambia wamwachie na baada ya kuachiwa, alianguka chini kama mzigo na ndipo walipogundua alikuwa hoi, maji yameingia puani na mdomoni. Hayo ni baadhi ya matukio makubwa yaliyomkuta Baby Madaha kwenye filamu hiyo ya The Gal Gladder. Anasema filamu hiyo anaamini itaendelea kuwa kumbukumbu kwa maisha yake kutokana na mikasa mikubwa iliyomkuta.

OFISI ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) ni Taasisi ...

foto
Mwandishi: Mohamed Musa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi