loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Tigo yachangia maabara sekondari

Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja wa Tigo Kanda ya Mtwara, Daniel Mainoya, alisema kampuni hiyo inaamini katika kuwapatia watoto mazingira bora ya kusomea, ili kuwajengea uwezo wa kuwa wananchi wanaowajibika na kuzalisha ipasavyo.

“Hii ni muhimu sana hasa katika kujifunza masomo ya sayansi, ni muhimu kwa watoto wetu kupewa vifaa vinavyotakiwa, ili kupata uelewa si wa kinadharia tu, bali uzoefu wa namna ya kujifunza masomo ya sayansi kama Baolojia, Kemia na Fizikia,” alisema Mainoya na kuongeza kuwa Tigo imeamua kutoa msaada huo ili kuinua elimu nchini.

Mtwara ni moja ya wilaya sita za Mkoa wa Mtwara, yenye jumla ya shule za sekondari 42 zinazoendeshwa na serikali, huku asilimia 18 tu ya shule hizo zikiwa na maabara za Fizikia, Kemia na Baolojia.

Maabara 43 zinahitajika katika sekondari mbali mbali Mtwara. Wilaya zingine za mkoa huo ni Newala, Tandahimba, Nanyumbu na Masasi.

Rais Jakaya Kikwete aliagiza mapema mwaka huu kuwa shule zote za sekondari za kata nchini, lazima ziwe na vyumba vitatu vya maabara ifikapo Novemba 30, mwaka huu. Hii ina maana zimesalia siku 15 tu kufikia tarehe ya mwisho ya agizo hilo.

foto
Mwandishi: Regina Kumba

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi