loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tiketi za elektroniki safi Ligi Kuu

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisa Habari na Mwasiliano wa TFF, Boniface Wambura, mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara kuwania ubingwa wa Bara unaanza Jumamosi kwa mechi tano katika miji ya Bukoba, Dar es Salaam, Tanga wakati mechi ya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting inahamishiwa uwanja mwingine.

Wambura alisema Ashanti United itacheza na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Coastal Union itacheza na Oljoro JKT katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wakati Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Azam FC na Mtibwa Sugar.

Alisema Jumapili kutakuwa na mechi kati ya JKT Ruvu na Mgambo Shooting itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex wakati Simba na Rhino Rangers zitaumana kwenye Uwanja wa Taifa.

Ofisa Habari huyo wa TFF alisema mechi ya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting iliyokuwa ichezwe Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine inahamishiwa uwanja mwingine kwa vile huo bado nyasi zake ambazo zimepangwa hivi karibuni hazijawa tayari kuhimili mechi hiyo.

“Hivyo Tanzania Prisons inatakiwa kutafuta uwanja mwingine unaokidhi viwango vinavyotakiwa kwa ajili ya mechi hiyo, na nyingine dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa Januari 29, mwaka huu,” alisema Wambura.

Yanga ambao ndio mabingwa watetezi, ndio wanaongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 28, wakifuatiwa na Azam FC na Mbeya City zenye pointi 27 kila moja wakati Simba iko nafasi ya nne ikiwa na pointi 24.

Mabingwa hao watetezi wanatarajiwa kurejea nchini kesho wakitokea Antalya nchini Uturuki ambako wako huko kwa takriban wiki mbili wakijifua, wakati Simba, Azam na Mbeya City zilishiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar na zimekuwa katika mazoezi katika miji yao ya Dar es Salaam na Mbeya.

Katika hatua nyingine, Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Boniface Wambura amesema Shirikisho la Soka Afrika (CAF), limeteua Watanzania Alfred Rwiza na Lina Kessy kuwa makamishna wa mechi za shirikisho hilo zitakazochezwa wikiendi ya Februari 14, mwaka huu.

Wambura alisema Rwiza ameteuliwa kusimamia mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Cote d’Or ya Shelisheli na Kabuscorp de Palanca ya Angola.

Alisema mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya mchujo itafanyika Shelisheli na itachezeshwa na waamuzi kutoka Madagascar wakiongozwa na Abdoul Kanoso. Waamuzi wengine ni Basile Rambeloson, Augustin Herinirina na Andofetra Rakotojaona.

Naye Kessy atakuwa kamishna wa mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Rwanda na Kenya itakayochezwa jijini Kigali. Waamuzi wa mechi hiyo wanatoka Cameroon. Mwamuzi wa kati ni Sylvie Abou wakati wasaidizi wake ni Winnie li Koudangbe, Lum Rochelle na Jeanne Ekoumou.

KOCHA wa timu ya taifa, ‘Taifa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi