loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Timu za Madola zatamba zimeiva

Katika michezo hiyo, Tanzania itashiriki katika michezo ya ngumi, riadha, kunyanyua vitu vizito, mpira wa meza, judo, kuogelea na baiskeli.

Wanamichezo watakaoshiriki mashindano hayo walipiga kambi katika nchi za Uturuki, China, New Zealand na Ethiopia, katika jitihada zinazofanywa na Serikali za kukuza na kuendeleza sekta ya michezo nchini kupitia mpango wa Diplomasia ya Michezo.

Akizungumza baada ya kuwasili nchini jana wakitokea Ethiopia, Kocha wa timu ya riadha aliyefuatana na wachezaji wanane, Shaban Hiiti alisema ana imani kubwa na wachezaji wake kuwa watailetea heshima Taifa kwa kuwa mazoezi waliyoyapata wakiwa Ethiopia yamewajengea uwezo mkubwa.

Hiiti aliongeza kuwa walipokuwa Ethiopia kwa mazoezi, wamejifunza mbinu mbalimbali kutokana na kuwa na programu za kuwajengea uwezo wachezaji wake.

“Ni matumaini yangu wachezaji hawa walioteuliwa kujiunga na wenzao waliokuwa mazoezini katika nchini zingine ambapo wanamichezo wetu walienda kwa ajili ya mazoezi, wataliletea Taifa letu heshima kubwa kwani wamepikwa wakapikika,” alisema kocha Hiiti.

Aidha, alisema uwepo wa mazingira mazuri na vifaa bora vya mazoezi, kumechangia kwa kiasi kikubwa kuinua ubora wa wanariadha hao ambao wamefanya mazoezi kwa takribani miezi miwili Ethiopia.

Kwa upande wake, mmoja wa wanariadha katika kikosi hicho, Alphonce Felix alisema anajisikia faraja kuwa miongoni mwa wanamichezo watakaoiwakilisha nchi katika Michezo ya Madola.

Alphonce alisema atatumia ujuzi alioupata Ethiopia kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo. Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Shirikisho na Ngumi Tanzania (BFT), Makore Mashaga alithibitisha kurejea kwa mabondia wa timu ya Taifa kutoka China na Uturuki na kueleza kuwa tayari wamejiunga na wachezaji wengine katika kambi iliyoandaliwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) iliyoko Kibaha.

“Mabondia hao walirudi juzi saa nane usiku na kupelekwa moja kwa moja kwenye kambi iliyoko kwenye shule za Filbert Bayi mjini Kibaha. Tuna imani kwamba wameimarika vizuri tayari kwa safari,” alisema.

Mabondia hao ni Joseph Martine, Emilian Patrick, Fabian Charles na Kocha Jonas Mwakipesile. Mashaga alisema wengine waliokwenda China wanatarajiwa kurejea Ijumaa kuungana na wenzao kambini.

Hao ni Seleman Kidunda, Nasser Mafuru, Mohamed Furahisha, Ezra Paulo na Hemed Hakim.

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ...

foto
Mwandishi: Waandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi