loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TPSF yataka kauli sera kuboresha uchumi

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya sekta Binafsi (TPSF) Godfrey Simbeye akizungumza mwishoni mwa wiki alisema ushauri wao kisera unaiweka nchi katika mazingira mazuri ya biashara.

Akizungumza wakati wa kufunga rasmi pazia la BEST AC, taasisi inayosaidia ushawishi katika kuboresha mazingira nchini, Simbeye alisema, mchango wa sekta binafsi katika kufanya mazingira ya biashara kuwa mazuri unatakiwa kutiliwa maanani katika ngazi zote za maendeleo kwa manufaa ya umma.

Mtendaji huyo pia alishukuru kuwepo kwa BEST AC kwa miaka kumi na kusema imechangia sana kuboresha mazingira kufuatia ufadhili wake katika masuala ya utafiti wa masuala yanayokwamisha mazingira bora ya ufanyaji biashara kwa lengo la kujenga uelewa na ushawishi wa mabadiliko katika sera na sheria.

Alisema ni matumaini yake kwamba mradi mwingine unaorithi BEST AC utaendelea pale ulipoachia hasa tatizo la urasimu.

“BEST AC imekuwapo kwa miaka 10 na nakiri kwamba hali ya kisera na uendeshaji wa sekta binafsi kwa sasa sivyo ilivyo wakati inaanza mwaka 2004, shukurani kwa mradi huu,” alisema.

WIZARA ya Habari, Utamaduni, Sanaa na ...

foto
Mwandishi: Beda Msimbe

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi