loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TRA Dodoma kukusanya bil. 37/- mwaka mmoja ujao

Meneja wa TRA Mkoa wa Dodoma , Thadey Kaliza alisema hayo jana katika mkutano wake na waandishi wa habari juu ya Wiki ya Mlipa Kodi na kuwataka wafanyabiashara kuona fahari kutoa kodi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Alisema katika mwaka huu wa fedha Serikali imewapangia mkoa huo kukusanya kiasi cha Sh bilioni 37 na kuongeza kuwa hiyo ni changamoto kubwa kwao.

Kaliza alisema mwaka uliopita Mkoa wa Dodoma ulipangiwa kukusanya jumla ya Sh bilioni 24.5 sawa na asilimia 93.5 huku lengo likiwa ni kukusanya bilioni 26.

Aidha alisema ongezeo hilo la mwaka huu, TRA kutakiwa kukusanya Sh bilioni 37 ni sawa na asilimia 10.

Alisema Watanzania wengi hawajisikii fahari kulipa kodi kwa faida ya maendeleo ya Taifa na badala yake wanaona ufahari kukwepa kulipa kodi.

Aliwataka Watanzania kujenga utamaduni wa kudai risiti pindi wanaponunua bidhaa mbalimbali ili kusaidia nchi kukusanya mapato.

Alisema taaluma ya kodi ina changamoto nyingi lakini cha msingi ni kuangalia jinsi gani walipa kodi wanavyoangalia suala hilo na lina faida gani kwao.

Alisema ni muhimu kwa wafanyabiashara kuwa na mashine unakuwa na uhakika na kile unachokipata katika biashara.

MWENYEKITI wa Taasisi za Sekta Binafsi ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi