loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TTB yaweka mikakati kukuza pato la utalii

Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB, Devotha Mdachi aliyasema hayo mwishoni mwa wiki Dar es Salaam alipokuwa akitoa tathimini ya Maonesho ya Utalii ya Kimataifa yaliyomalizika Dar es Salaam, juzi.

Mdachi alisema pamoja na mikakati mingine wamedhamiria kufungua matawi ya ofisi za vivutio vya utalii katika maeneo mbalimbali nchini katika kuhakikisha utalii wa ndani pia unakua.

Alisema sekta hiyo kwa sasa inachangiwa zaidi na watalii kutoka mataifa mengine duniani ambapo mchango wa Watanzania wenyewe umekuwa mdogo hivyo mikakati madhubuti inatakiwa kuwekwa katika kuhakikisha utalii wa ndani unakua na kuchangia ipasavyo katika sekta husika.

“Tumekuwa tukifanya jitihada mbalimbali katika kuhakikisha sekta hii inachangia vizuri katika pato la taifa na kwa sasa tunaendelea na mikakati kabambe na malengo ni kuona sekta hii inachangia kwa asilimia 30 katika miaka mitano ijayo.

“Tunaendelea kufungua matawi ya ofisi zetu za vivutio katika maeneo mbalimbali na hili ni katika katika kuhakikisha tunaongeza hamasa kwa Watanzania kutembelea vivutio vilivyopo na kuongeza pato la sekta hii,” alisema Mdachi.

Akizungumzia Maonesho ya Kimataifa ya Utaliii (SITE) yaliyomalizika hivi karibuni alisema yamefanyika kwa mafanikio makubwa ambapo zaidi ya washiriki 1,000 walihudhuria.

Maonesho hayo ya Utalii ya Kimataifa yaliyofanyika nchini kwa siku nne na kumalizika mwishoni mwa wiki Dar es Salaam yatakuwa yanafanyika kila mwaka ambapo kupitia maonesho hayo Sekta ya Utalii inatarajiwa kuwa na mchango mkubwa zaidi katika pato la taifa katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi