loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TTCL kuunganisha watu 3,700 Morogoro Vijijini

Hayo yalibainishwa juzi na Mkurugenzi wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa TTCL, Juvenali Utafi katika hafla ya uzinduzi wa mnara huo uliojengwa katika kijiji cha Kisanga stendi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa TTCL kuwa, uzinduzi wa mnara huo ni sehemu ya mpango wa serikali wa kuhakikisha wananchi wanafikiwa na huduma za mawasiliano, hususan waishio vijijini.

Hata hivyo alisema TTCL imeanza kutekeleza miradi ya ujenzi wa minara katika vijiji 20 hapa nchini ambayo itagharimu kiasi cha Sh bilioni 3.7 ili kuwawezesha wananchi waishio vijijini kuwa na mawasiliano ya uhakika ambapo kwa mkoa wa Morogoro mradi huo umetekelezwa katika kata ya Tununguo na ya Iragua iliyopo wilayani Ulanga.

Naye Alfred Shayo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo amewataka wananchi wa maeneo hayo kutunza miundombinu hiyo na kuwafichua wale wote watakaobainika kuihujumu.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi