loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tuache bei za kukomoana wakati wa Ramadhani

Utafiti uliofanywa katika maeneo hayo, umebaini kuwa baadhi ya bidhaa zilizopandishwa bei ni mkungu wa ndizi kutoka Sh 6,000 hadi 10,000, fungu la viazi vitamu na muhogo kutoka Sh 1,000 hadi 2,000, huku gunia la viazi ambalo awali lilikuwa linauzwa kwa Sh 40,000, sasa linauzwa kwa Sh 60,000.

Tunapenda kuungana na viongozi wetu, wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki na Shekhe wa Mkoa huo, Alhad Mussa Salum kuwasihi wafanyabiashara katika maeneo hayo na mengine nchini, kuachana na tamaa hiyo inayopitiliza ya kutaka kupata kipato cha hali ya juu katika muda mfupi, hususan kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Tunafahamu kwamba lengo kuu la kila mfanyabiashara ni kutengeneza faida.

Lakini ni ukweli pia kwamba katika harakati za kutengeneza faida, hawana budi pia kuwafikiria wateja wao kwa kuwapatia bei, ambayo wanaweza kuimudu, huku pia kwa upande wao kupata faida ya kuendeleza biashara zao.

Katika hili tunapenda kuwakumbusha wafanyabiashara, kwamba wateja wanawategemea wao na pia wao wanawategemea wateja, kwa maana kwamba wote wanategemeana kwa umuhimu wao katika nafasi zao za mlaji na mfanyabiashara.

Hivi utajisikiaje kama unauza bidhaa za vyakula sokoni, dukani au mahali popote pale kwa bei ya juu na halafu wateja hawaji kwako na kwenda kutafuta bidhaa hiyo hiyo maeneo mengine ; au kutokana na kukosa fedha za kufanya manunuzi hayo?

Sote tunafahamu fika kwamba wenzetu Waislamu katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, hufunga kwa sababu ni mwezi wa toba na nyakati za jioni hufuturu na bidhaa zilizotajwa, ndizo haswa hutumika kwa wingi nyakati hizi.

Kwa nini wafanyabiashara wetu, msitumie wingi wa mahitaji ya bidhaa hizo kuuza zaidi na kupata faida zaidi pia, badala ya kuwakomoa kwa kuwapandishia bei wenzetu walio katika mfungo?

Kwa nini tunataka kuwakwaza, badala ya kuwasaidia wenzetu hao, kukamilisha toba katika Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani. Kwa nini tukitumie kipindi hiki kwa kujitengenezea faida kubwa zaidi kwa kila hali, huku tukijua fika tunawaumiza wenzetu?

Tunawasihi katika kipindi hiki, tutangulize utu wetu mbele kwa kusaidiana katika kupatikana kwa bidhaa hizo kwa bei nafuu ili anayejaliwa kufunga kwa toba hii, asijisikie kuwa anapata adhabu.

Hili linawezekana tukiendeleza utamaduni wetu sisi Watanzania wa kushikamana katika shida na raha, huku tukilinda amani na utulivu wetu.

FUKUTO la Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani linazidi ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi