loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tuimarishe mapambano Ukimwi bado upo

Kiwango hicho ni zaidi ya kiasi cha wastani wa mkoa huo cha asilimia 5.9 na kiwango cha taifa cha asilimia 5.1. Wilaya hiyo yenye wakazi 354,000, kati yao wakazi 3000 wanatumia dawa za kufubaza Ukimwi (ARVs).

Akihutubia mamia ya wananchi mjini Mbinga hivi karibuni, kabla ya kuzindua kituo kipya cha mabasi mjini humo, Rais Jakaya Kikwete alieleza wazi bila kumung'unya maneno, kwamba wananchi wazingatie matumizi ya kondomu wakati wa kujamiana ili kuwanusuru na ugonjwa huo, ambao tiba yake bado haijapatikana duniani hadi sasa.

Aliwakumbusha kwamba haisaidii kujifanya mahodari wa kuwa na wapenzi wengi, tena bila kutumia kondomu, kwani ipo siku watanasa, jambo ambalo halitamsaidia yeye mhusika wala taifa. ''Ndege mjanja hunasa kwenye tundu bovu'' alionya Rais Kikwete katika hotuba yake.

Tunamuunga mkono Rais Kikwete, kwa kuwakumbusha wananchi juu ya umuhimu wa kuchukua hatua za makusudi, kujilinda na ugonjwa huo bila kufanya ajizi, kwani kinyume chake wananchi wetu, hususani nguvu kazi ya vijana, itapotea na kuliacha taifa katika hali mbaya kwenye harakati za kuendeleza gurudumu la kujiletea maendeleo ya kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na kijamii.

Ni dhahiri kuwa takwimu za maambukizi ya Ukimwi katika wilaya hiyo, zinataka kila mmoja wetu kuchukua kila aina ya tahadhari ili kuepuka ngono zembe, ambazo sote tunafahamu fika kwamba ndiyo chanzo kikuu cha kuenea kwa kasi kwa ugonjwa huo hatari.

Miaka ya 1980 Ukimwi ulipobisha hodi katika taifa letu kwa mara ya kwanza, kulikuwa na hali ya kutoelewa vizuri juu ya ugonjwa huo, maambukizi yake na namna ya kujikinga huku kukiwa na unyanyapaa wa hali ya juu, kwa mtu aliyekubwa na ugonjwa huo.

Lakini ni ukweli pia kwamba juhudi za kitaifa na kimataifa, zimewezesha kutoa elimu ya kutosha juu ya ugonjwa huo na jinsi ya kukabiliana nao, kiasi kwamba watu sasa wanaweza kuuzungumzia hadharani bila kuogopa au hawawezi kunyanyapaliwa tena, tofauti na hapo awali.

Wananchi pia wanafahamu kwamba anayeathirika na ugonjwa huo sasa, haimaanishi kwamba tayari anasubiri kufa, bali anaweza bado akaishi na kufanya shughuli nyingine za kujikimu kama watu wengine, huku akitumia dawa za ARVs hadi hapo Mungu atakavyoamua vinginevyo.

Tunaungana na Rais Kikwete, kuwa wale ambao wanaishi na virusi vya Ukimwi, wasisambaze kwa wengine, bali waishi kwa kufuata ushauri wa wataalamu ili kwa pamoja tuweze kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo.

Hili linawezekana kama upo mshikamano kati ya wananchi, wataalamu na washika dau wengine katika vita dhidi ya Ukimwi ili kwa pamoja tuweze kufikia lengo la kuwa na Tanzania isiyokuwa na Ukimwi.

Hili linawezekana kama wenzetu wa Mbinga na sisi wengine katika maeneo mbalimbali hapa nchini, tukidhamiria kwa dhati kukabiliana na hali hiyo kwa nguvu na uwezo wetu wote.

RIPOTI ya 15 kuhusu uchumi wa Tanzania ya ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi