loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tukabili ajali za bodaboda kwa nguvu zote

Lakini ni ukweli pia kwamba usafiri huo umekuja na mambo yake pia. Kubwa likiwa ni ajali za wanaotumia vyombo hivyo pamoja na abiria wao.

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga alisema mapema wiki hii katika tukio la uzunduzi wa mafuta mapya ya kuimarisha na kulainisha injini za pikipiki kwamba usafiri huo umesababisha jumla ya vifo 423 katika kipindi cha miezi sita iliyopita.

Katika kipindi hicho pia kwa Mkoa wa Dar es Salaam pekee, watumiaji wa bodaboda 1,303 walipata ajali ambapo 83 kati yao walipoteza maisha.

Taarifa hizi zinatupa taswira ya kukosa amani na usalama kwa watumiaji wa usafiri huu ambao hivi sasa upo karibu kila kona ya nchi yetu.

Inasadikiwa kwamba katika kila hospitali ya ngazi za wilaya, mkoa na hata rufaa idadi ya majeruhi wanaotokana na ajali za pikipiki huwa inaongezeka kila kukicha huku juhudi za kudhibiti ajali hizo kwa watumiaji zikiwa haziendani na kasi ya kukabiliana na janga hilo.

Sababu kubwa zinazotolewa ni pamoja na uzembe wa madereva wa kutozingatia alama za usalama barabarani lakini pia mwendo kasi wa madereva wake.

Hivi tutaendelea na hali hii mpaka lini? Je tutaendelea kuzalisha vilema wa viungo mbalimbali na kusababisha upotevu wa maisha mpaka lini? Hatutaki kuamini kwamba sasa tumeshafikia upeo wa kufikiri na kushindwa kuidhibiti hali hiyo.

Ukweli ni kwamba bado uwezo huo upo na linalokosekana ni ukosefu wa mikakati muhimu kwanza ya mafunzo kwa madereva wote kabla ya kupewa leseni za kutumia vyombo hivyo.

Hivi kama upande wa magari upo utaratibu wa mafunzo ya udereva kabla ya mhusika kupewa leseni kwa nini mbinu hizohizo zisitumike kwa bodaboda? Kinachoshindikana hapa ni kitu gani kama vyombo hivyo vinapita barabarani kama yalivyo magari? Mara nyingi hushuhudia ukaguzi wa leseni kwa madereva wa magari ya aina yote toka madogo hadi makubwa ya kubeba mizigo.

Kwa nini ukaguzi huo ni nadra sana kwa bodabaoda ambazo huongezeka barabarani kila kukicha? Kama ukaguzi wa mara kwa mara haupo tunashangaa nini kuwepo kwa ongezeko la ajali barabarani?

Tungependa kuwashauri madereva wa bodaboda, polisi na wananchi kwa ujumla kushirikiana katika kukabili hali hiyo ya ajali hadi kufikia kiwango cha kuzidhibiti ili usafiri huo, uwe na manufaa kwa kila mmoja anayeutumia na siyo kuwa sababu ya kutengeneza vilema na vifo kila siku. Hili linawezekana na tuseme hapana kwa ajali hizi.

RIPOTI ya 15 kuhusu uchumi wa Tanzania ya ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi