loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tumbi waishtaki Wizara ya Afya kwa Kinana

Aidha imedaiwa kwamba fedha kwa ajili ya kukamilisha awamu ya pili ya ujenzi wa jengo kwa ajili ya upanuzi wa hospitali hiyo hazijatolewa.

Hayo yalisemwa na Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Peter Dattani wakati akimpa taarifa za hospitali hiyo Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Abdulrahman Kinana ambaye yupo katika ziara ya Mkoa wa Pwani.

Daktari huyo alisema kwamba miaka mitatu iliyopita Wizara ya Afya iliwataka kuandaa chumba cha ICU kwa ahadi kuwa itatoa vifaa vyote, ahadi ambayo haijatekelezwa.

Daktari huyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Huduma za Afya hospitalini hapo alisema endapo chumba hicho kingekamilika, hospitali hiyo isingewahamishia wagonjwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

“ Hatuna tatizo na kuwapeleka wagonjwa Muhimbili kwanza wanatupunguzia kazi, lakini nusu yao hufariki wakiwa njiani kwa sababu wanakuwa na hali mbaya. Kama chumba hiki kingekuwa na vifaa wagonjwa tungeweza kuokoa watu wengi.”

Kuhusu ujenzi wa jengo jipya la upanuzi wa hospitali, Dattani alisema kuwa walikamilisha ujenzi wa jengo moja lakini wakashindwa kupata fedha kukamilisha ujenzi wa jengo la pili.

Kinana alionesha kusikitishwa na hali hiyo na kusema ipo haja ya kurejesha nidhamu ya utendaji serikalini.

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wananchi ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Kibaha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi