loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tunatambua juhudi za taasisi za dini kuleta maendeleo -RC

Mkuu huyo wa wilaya aliyasema hayo juzi wakati alipokuwa amemwakilisha Mkuu wa Mkoa, Dk Rajab Rutengwe, katika maadhimisho ya kumbukumbu ya Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya yaliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha Ahmadiyya kilichopo mjini Morogoro.

Maadhimisho hayo ni sehemu ya kumkumbuka mwanzilishi wa jumuiya hiyo, Hadhrat Mirza Ghulam Ahmed wa Qadiani Masihi na Mahdi. Kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya, Serikali wanatambua mchango wa jumuiya hiyo iliyotolewa na kuendelea kutolewa kwa jamii mkoani Morogoro na nje ya Morogoro.

Hata hivyo, aliitaja michango iliyotolewa na jumuiya hiyo ni uchimbaji wa visima vya maji safi na salama katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na Arusha ambayo ni sehemu yao ya kuiunga mkono serikali katika kupunguza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama.

Kabla ya kumkaribisha mkuu wa wilaya, Shehe wa Mkoa wa Morogoro wa Jumuiya hiyo, Bakari Abeid alisema lengo la maadhimisho hayo ni kuwakumbusha waumini kwa kutenda mambo mema bila kubagua mtu kama walivyokuwa wakifanya mitume wote waliopita.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kihonda Maghorofani, Lidya Mbiaji, akitoa salamu za wananchi wa kata hiyo aliwataka Watanzania kuendelea kuwa wamoja.

Pia aliwashauri viongozi wa dini kuhubiri mambo mema ambayo hayatasababisha uvunjifu wa amani kwa vile mitume wote waliopita wahubiri amani kwa mataifa yote bila kujali dini wala itikadi ya mtu.

RAIS John Magufuli amesema Manispaa ya Ilala imepandishwa ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi