loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tunaungana na Rais Kikwete kuwapongeza watafi ti wa IHI

Rais Kikwete alitoa pongezi wakati kundi la watafiti wa IHI lilipokwenda kumtembelea katika makazi yake huko Malabo, Equatorial Guinea (EG) ambako anahudhuria mkutano wa Afrika wa tabia nchi.

Watafiti hao wapo nchini humo kwa mwaliko wa serikali ya nchi hiyo kwa ajili ya kutoa msaada wa kitaalamu katika utekelezaji wa mradi wa utafiti wa chanjo ya malaria iitwayo PfSPZ.

Pamoja na kushawishika kushirikiana na Rais Kikwete katika kutoa pongezi hizo sisi wa HabariLEO Jumapili tunapenda kuwashauri watafiti wetu hao kutobweteka na pongezi hizo, kwani wakifanya hivyo wanaweza kujikuta `wanavimba’ kichwa na hatimaye kujiangusha wenyewe.

Ni ukweli usiopingika kwamba kutokana na ujuzi wao ndio maana serikali ya Equatorial Guinea wameitwa nchini huko kuwafunza wenzao maarifa sahihi ya kukabiliana na mbu na utafiti wa chanjo ya malaria.

Hatuna shaka na kazi inayofanywa na IHI, hasa kwa kuzingatia kuwa wameshafanya tafiti mbalimbali za afya nchini Tanzania katika uzoefu wo wa miaka zaidi ya 50.

Sote tunajua kwamba moja ya mafanikio yao ni utafiti uliosababisha vyandarua vyenye dawa kutumika kama moja wapo ya njia za kujikinga na malaria nchini Tanzania.

Na kutokana na vyandarua hivyo na kampeni ya kila mtu kuwa nacho imefanya hata foleni za kwenda kumuona daktari kupungua huku tukijua kwamba taifa lenye siha njema ndilo lenye uchumi mzuri.

Kutokana na kazi nzuri ambayo taasisi hii inafanya katika kukabiliana na mbu wa malaria, tena kwa kushirikiana na mataifa na taasisi nyingine, kitendo cha kualikwa kusaidia nchi nyingine ni kitu cha kujinua mno.

Hivyo tunaamini kama ambavyo wameaminiwa kutokana na utaalamu wao, wataendelea kutimiza vyema majukumu yao kwa faida ya mtafiti mmoja moja, kwa taasisi lakini pia kwa sifa na heshima ya taifa lao.

Kwa kifupi, tunamaanisha wajikite zaidi katika kufanikisha kile kilichowapeleka Guinea ili kuithibitishia Dunia kwamba, Watanzania nasi tunaweza.

Tunaamini ushirikano huu ni mmoja ya mfano wa mashirikano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ili kutafuta njia bora za kukinga maradhi katika jamii. Pia tunaamini vilevile ni moja ya kielelezo kizuri cha jinsi gani nchi za kusini zinaweza kushirikiana katika taaluma mbalimbali (south south corporation).

Pamoja na kupata fursa ya kukutana na Rais Kikwete mjini Malabo na kumueleza kuhusu kazi wanayofanya na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo, sehemu kubwa ya heshima wanayobeba ni wao na kama taifa tunawashukuru kwa kutulindia heshima yetu.

Aidha, tungelipenda serikali kuwasikiliza waliokwenda Malabo kuhusu suala la kusahilisha mashirikano kati ya nchi mbili za Tanzania na Equatorial Guinea kupitia Wizara za Afya na Tume za Sayansi na teknolojia ili utelekezaji wa ushirikiano uwe bora zaidi kwa lengo la kunufaisha nchi zote mbili.

Tunaamini kama tunavyoamini katika pongezi kwamba mashirikiano haya yakipatikana yatatoa fursa kwa watanzania kutobweteka hivyo kuwafunza wenzao na wao kujifunza kutokana na mashirikiano hayo.

UCHAGUZI Mkuu wa madiwani, wabunge, wawakilishi, Rais wa Zanzibar na ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi