loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tunduru wahimizwa kukusanya maduhuli ya serikali

Hayo yalibainishwa wilayani hapa jana na Kamishna wa Madini, Paul Masanja, wakati akizungumza na wafanyakazi wa ofisi hiyo, katika ziara ya Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, Eliakim Maswi, wilayani hapo.

Alisema kutokana na wingi na utajiri wa madini hasa vito katika wilaya hiyo, ofisi hiyo ilipaswa kukusanya maduhuli na kufikisha lengo lililowekwa na serikali la Sh milioni 500 kwa mwaka, lakini matokeo yake, kiwango hicho kimeshindwa kufikiwa kwa asilimia kubwa.

“Tunduru ni moja ya wilaya zinazotuangusha katika eneo la ukusanyaji wa maduhuli, licha ya uwepo mkubwa wa migodi ya madini na vito. Lakini nyie mko hapa mnaachia wachimba madini wanakimbilia nchi jirani hamfanyi lolote,” alisema.

Alisema Serikali haitokubaliana na utendaji wa aina hiyo na kwamba ofisi hiyo ni lazima ifikishe kiwango hicho cha Sh milioni 500 kwa mwaka cha ukusanyaji wa maduhuli.

Awali Ofisa Madini mkazi wa wilaya ya Tunduru, Frederick Mwanjisi, alisema mwaka huu wamejiwekea lengo la kukusanya maduhuli ya Sh milioni 500 na hadi kufikia mwaka huu wa fedha tayari wamekusanya Sh milioni 20.7.

ABIRIA 80 wakiwemo watalii wameshuka Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa ...

foto
Mwandishi: Halima Mlacha, Tunduru

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi