loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tunu Pinda ahimiza vicoba kupunguza umasikini

Hayo yalisemwa Mjini hapa jana na Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda wakati wa uzinduzi wa kikundi cha Vicoba cha watumishi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Makao Makuu.

Alisema wananchi wanatakiwa kuchangamkia fursa kwa kujiunga kwenye vikundi vya kuweka na kukopa kwani mfumo huo umeonesha mafanikio makubwa katika mikoa mingi hapa nchini.

Alisema mafanikio hayo yanatokana na ushirikishwaji katika kuanzisha na kusimamia vikundi jambo ambalo limewavutia wananchi wengi.

Mama Pinda alisema anatumaini kuwa vicoba wataendelea kuimarisha mfumo wa kuanzisha vikundi vipya, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya uongozi, kibenki na mbinu mbalimbali za kibiashara, kimaisha na nidhamu ya kutumia fedha.

Alisema licha ya Vicoba kukabiliwa na changamoto mbalimbali ni muhimu kwa uongozi kuhakikisha kunakuwa na tahadhari za mapema ili vikundi viwe salama.

Alizitaja changamoto hizo kuwa ni kuibuka kwa wadau wasiofuata kanuni za Vicoba, namna ya kutunza kumbukumbu, gharama za uendeshaji ofisi, miundo tofauti ya taasisi zinazojihusisha na jamii na ukosefu wa fedha za kutathimini mpango.

Akisoma risala ya kikundi cha Vicoba, Lucy Rutahinirwa alisema kikundi hicho kilianzishwa Septemba 13, mwaka jana na sasa kina wanachama 60 ambapo kati yao wanawake ni 46 na wanaume ni 14.

Alisema wanachama wa kikundi hicho wameweza kununua hisa zenye thamani ya Sh milioni 13.6 ambao ndiyo mtaji katika kutimiza lengo la kujiimarisha kiuchumi jumla ya wanachama 48 wamekopeshwa mkopo unaofikia Sh milioni 22.5 na marejesho ya mkopo yanaendelea vizuri.

Alisema lengo la kikundi hicho ni kuona wanachama wanaongeza hisa ili kuwa na mtaji mkubwa zaidi wa kuendesha kikundi.

“Bado tunaendelea kushawishi watumishi wenzetu nchi nzima ambao sio wanachama kujiunga na Vicoba kama njia ya kuongeza kipato na kuwajengea wafanyakazi uwezo mkubwa wa kujiimarisha zaidi kiuchumi kwa kupewa mikopo yenye masharti nafuu,” alisema.

Katika uzinduzi huo, jumla ya Sh milioni 18 zikiwa ni ahadi na fedha taslimu zilipatikana ambapo mke wa Waziri Mkuu aliahidi kutoa Sh milioni tano na Rais wa Vicoba Tanzania Devota Likokola aliahidi kutoa Sh milioni mbili.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi